Header Ads Widget

DOLA BILIONI 1.3 ZAWEKEZWA KATIKA ZAO LA PARACHICHI



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma


MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya The Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT)Geofrey Kilenga amesema jumla ya Dola bilioni 1.3 zimewekezwa katika zao la parachichi kupitia wabia waliowekeza ambao ni wakulima  wa zao hio duniani kote 


Kilenga amesema hayo jijini hapa leo,Agosti 7,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Avocado kwenye maonesho ya wakulima maarufu kama nanenane katika viwanja vya Nzuguni ambapo alisema banda la avocado limeshirikisha washiriki wapatao 60 na mabanda yapo 18 kutoka katika nchi mbalimbali ,Ulaya ambapo ni Finland lakini vilevile Afrika kusini.



"Hapa kuna watu wanawezesha wakulima kama wewe upo mjini huwezi kulima wanaweza kukupa utaratibu na wewe wakakutolea huduma ya kulima lakini kuna ambao wananunua mazao mbalimbali yanayokwenda nje na vilevile kuna wasindikaji wanaweza kuongeza thamani humu ndani hivyo hii ni fursa kwa wananchi kuja kujifunza na kupata ujuzi namna ya kumiliki mashamba ya parachichi na kujiingizia kipato.


Ametaja lengo kubwa la kuwepo hapo kuwa wapo karibu mnyororo mzima kuanzia wakulima ambao wanazalisha avocado lakini vilevile ambao ni watanzania wakulima wadogo kunawakulima ambao  wanamashamba makubwa ili kutoa elimu hata kwa watu ambao hawana mashamba makubwa kuweza kulima kilimo cha parachichi.


"Sasa baadhi ya watu pengine watakuwa wanajiuliza parachichi ni nini hapa kunamafano wa zao linazalishwa hapa nchini kuanzia Njombe,Iringa,Ruvuma hayo ni maeneo maarufu lakini sasa hivi lina kwenda mpaka mkoa wa kigoma 

Morogoro,Sumbawanga na Rukwa ,Arusha kilimanjaro pia wanazalisha na watu wanapata faida"amesema Kilenga.


Amesema kuwa zao la parachichi ni zao lenye faida duniani kote kwani limeongezewa thamani kwa kutengeneza mafuta na bidhaa mbalimbali. 


Hata hivyo amesema mbali na uzalishaji wameanza kuongeza thamani katika zao hilo kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo kusindika mafuta ya avocado na yanasindika Tanzania.


Kwaupande wake Beno Mgaya kutoka Taasisi ya Afrifarm ambaye ni mkulima maarufu  Tanzania ambaye sasa hivi anafanyakazi  na maelfu ya wakulima na ni  baada ya kupewa mafunzo kupitia ubia wa wa zao hilo amesema anafanya kazi, katika mikoa tisa ambayo ni ,Ruvuma,Njombe,Mbeya,Rukwa,Kigoma,Morogoro na Dodoma.



Amesema yao  kubwa ni kuangalia jjnsi gani wanawasaidia wenye kipato cha chini kuzalisha zao la parachichi kwasababu zao la parachichi ilikuweza kuzalisha lilikuwa linahitaji watu wenye fedha lakini wameingia hata kwenye kaya zile ambazo masikini ambazo hazijiwezi kabisa na ndivyo tulivyokutwa huko njombe tukiwa kwenye kaya hizo masikini.


"Hivyo tulivyoibuliwa sisi na sisi tumeibuka kwenda kuwainua wenzetu kwasababu,Zao la parachichi ili uweze kuzalisha kwa heka moja unakiwa uwe na milioni 1.5 mpaka milioni 2 kwa heka kuanzia uandaaji wa miche mashimo mbolea na kila kitu,"amesema Mgaya.



Lipita Mtimbila ni Meneja wa Kampuni ya Afrifarm amesema wamekuja na ubunifu wakuwaleta pamoja wadau wa mnyororo wa thamani wa zao za parachichi ili waweze kuzungumza fursa zilizopo kwenye zao la parachichi Tanzania.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI