MJUMBE wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha mapinduzi (CCM )Mkoa wa Iringa, Dk Tumaini Msowoya amewashauri wajumbe wa Baraza la Wazazi, Kata ya Mkwawa, Iringa Mjini kutochoka kutoa elimu kwa jamii kuhusu malezi.
Pia amewashauri kuhakikisha wanazihasisha familia zenye vijana walio na umri wa miaka 18 na kuendelea wajiandikishe kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.
Dk Tumaini Msowoya alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Baraza la Wazazi, Kata ya Mkwawa ambalo pamoja na mambo mengine lilielezea mikakati yake kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
"Taarifa yenu inaonyesha Jumuia ya Wazazi kwenye kata hii ipo hai, hongera sana. Tuendelee kupambana kwenye malezi, familia imara ndio msingi wa maadili kwenye jamii yetu," amesema Msowoya.
"Malengo ya chama chochote ni kushuka dola, daftari la kudumu la wapiga kura likifika Iringa tukajiandikishe sisi na tuhamasishe jamii yetu kwa makundi yote, vijana na wanawake na wanaume Ili uchaguzi ukifika, tukaipigis kura CCM,"
Awali, Katibu wa CCM Kata ya Mkwawa, Khalid alisema wanaendelea kuchapa kazi katika kuhakikisha, CCM inazoa mitaa yote kwenye kata hiyo.
0 Comments