Kituo cha Kudhibiti na Kujikinga na Majanga ya Magonjwa Afrika (Africa CDC) kimeutangaza ugonjwa wa homa ya nyani #Mpox kuwa janga la kimataifa.
Kwenye taarifa yake, mkurugenzi wa Afrika CDC, Jean Kaseya amesema ugonjwa huo unasambaa kwa kasi miongoni mwa nchi za Afrika hivyo msaada wa jumuiya ya kimataifa unahitajika kwa haraka.
Kwenye chapisho lake la Agosti 10 kwenye ukurasa wa mtandao wa X, Kaseya alisema Afrika ina chanjo 200,000 pekee huku mahitaji yakiwa chanjo milioni 10.
Tangu kuzuka kwa mlipuko wa ugonjwa huo mwanzo mwaka huu zaidi ya watu 13,700 wameripotiwa kuambukizwa huku vifo vikifikia zaidi ya 450 kwenye Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo pekee.
Virusi vya ugonjwa huo vimeripotiwa kusambaa kwenye nchi za Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kenye na Rwanda.
0 Comments