Header Ads Widget

DIRA MAENDELEO YA TAIFA 2050 KUJUMUISHA MAWAZO YA WANANCHI


NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Jamii imeaswa kujitokeza kushiriki kutoa maoni ya mpango wa maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 ili kujumuisha mawazo ya pamoja bila kujali tofauti zao za kidini wala kisiasa kwa maendeleo endelevu ya Taifa kwa miaka mingi ijayo.


Rai hiyo imetolewa na Mjumbe wa timu kuu ya kitaalam ya mpango wa dira ya Taifa ya mwaka 2050.


Mwana taaluma huyo ambaye pia ni mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam amesema dira ya maendeleo inalenga kukusanya maoni ya wananchi wote wala si ya Serikali wala chama chochote cha siasa.


Amewataka wananchi katika maeneo yao kuendelea kutoa maoni yao kuelekea maendeleo endelevu kwa miaka inayo kuanzia mwaka 2025 hadi mwaka 2050 kutokana na kwamba dira ya maendeleo inayoishia mwaka 2025 ilianza kutekelezwa tangu mwaka 2000.


Aidha amesema timu ya wataalam hao kutoka makao makuu imefika jijini Mbeya ili kusikiliza na kukusanya maoni ya wananchi kupitia kongamano maalum katika ukumbi wa Eden jijini humo, kupitia simu ya mkononi na makongamano kwenye maeneo mbalimbali ya wananchi ikiwemo kwenye ngazi za Halmashauri.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI