Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa rai kwa Watanzania kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa wanaofaa kwa maendeleo ya Taifa.
Dkt. Biteko amesema hayo leo Agosti 31, 2024 wakati wa NMB Bunge bonanza iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya John Merlin jijini Dodoma.
Amesema Tanzania inahitaji viongozi wenye maono na mapenzi na nchi hivyo ni jukumu la kila mtanzania kujiandaa kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi.
Akizungumzia bonanza hilo Dk. Biteko amesema hamasa kwa watanzania kuendelea kuchangia maendeleo huku akitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa jamii kiendeleza utamaduni wa kufanya mazoezi kwa afya.
Kwa upande wake Spika wa Bunge Dkt,Tulia Ackson amesema bonanza hilo litasaidia kuchangia ujenzi shule ya wavulana Bunge.
Amesema hatua hiyo itasaida kuleta usawa kwa watoto wote wa kiume na wa kike.
"Tulianza na shule ya sekondari ya wasichana na sasa Bunge linaenda kufanya hivyo hivyo kwa wavulana, tunahitaji kuwalea watoto wote kwa usawa kila mtoto ni muhimu, " amesisitiza
Pamoja na Mambo mengine bonanza hilo limeandaliwa na Benki ya NMB ambayo imetoa jumla ya shilingi milioni 50 kama mchango wa ujenzi wa shule ya wavulana ikiwa ni shukurani kwa jamii.
Naye Mwenyekiti wa Bunge Bonanza na Bunge Marathon Festo Sanga amesema bonanza hilo ni mataharisho ya kujipanga kwenye mashindano ya mabunge ya Afrika Mashariki.
Aidha amesema bonanza hilo linazidi kukua kila siku ambapo wameweza kuongeza tena taasisi zingine ambazo ni Wizara ya Nishati,Wizara ya Maji, Wizara ya Mariasili,
"Kama Spika wetu wa bunge alivyoagiza Bunge tujenge mahusiano mazuri na taasisi hivyo bonanza hili linakwenda kudumisha mahusiano mema, " Amesema Mwenyekiti Sanga
Na Kuongeza " Bonanza hilo linakwenda kuunga mkono juhudi za Viongozi wa juu wa serikali za kutaka jamii kufanya mazoezi ili kuondokana na magonjwa yasiyo ya lazima ambayo yamekuwa yakiigharimu serikali kutibu wananchi.
Mwisho.
0 Comments