Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Serikali Wilayani Njombe imesema ipo Haja ya wanafunzi kuvaa makoti ikiwa ni miongoni mwa sare kwani itasaidia kwa kiasi kukabiliana na changamoto ya baridi kali hasa majira ya Asubuhi kwani hali ni Mbaya.
Kauli hiyo inatolewa na mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa katika ziara yake ya Kikazi ya Kukagua ujenzi wa Miundombinu ya Vyoo na kwamba tayari kumeripotiwa athari ya baridi kwa baadhi ya wanafunzi mkoani Njombe.
Aidha Kasongwa ameridhishwa na Ukamilishwaji wa Ujenzi wa vyumba 49 vya madarasa na vyoo 120 katika halmashauri ya mji wa Njombe uliyogharimu shilingi Bilioni 1.4 kwa lengo la kuboresha miundombinu ya elimu katika shule za sekondari Mpechi,Mabatini na Njombe[NJOSS
Wakati mkuu wa wilaya akitaka mpango wa sare za makoti kwa wanafunzi kupitishwa mara moja ili kuwakinga watoto na athari za baridi ,wanafunzi nao kutoka shule tofauti akiwemo Frank Peter,Elia Shingwe na Marina Ngonyani wanasema baridi ni tatizo kubwa kwao huku pia wakisema maboresho hayo ya miundombinu yanaongeza ari ya kusoma kwa bidii.
Kwa upande wake Ofisa elimu halmashauri ya Mji wa Njombe Mwl Rehema Nswila anasema ujenzi wa vyoo 120 na madarasa 49 utakuwa na matokeo chanya kwa wanafunzi.
Baadhi ya Wakuu wa Shule akiwemo Brown Kiswaga Mkuu wa shule Mpechi sekondari na walimu wanasema motisha kwa walimu wa kujitolea ni muhimu huku wakishukuru kwa ujenzi wa Miundombinu hiyo.
Mikoa Mitatu ya Kusini mwa Tanzania ukiwemo mkoa wa Njombe,Mbeya na Iringa imekuwa na Baridi kali inayosababisha madhara makubwa kwa binadamu Wanyama na Mimea jambo ambalo hatua mbalimbali zinapaswa kuchukuliwa ili kupunguza athari hizo.
0 Comments