Header Ads Widget

WANANCHI DUMISHENI ULINZI ,AMANI NA UPENDO IRINGA .

 

Chesco Ng'umbi - Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya CF akizungumza na kuwaasa Wafanyakazi wa Kituo cha Mafuta cha Villa Energies Tanangozi.

Picha mbali mbali za Uzinduzi wa Kituo cha Mafuta cha Villa Energies Tanangozi.

Joseph Lyata - Mgeni rasmi  Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Iringa akikata utepe kufungua kuzindua miradi wa Kituo cha Mafuta cha Villa Energies Tanangozi na kuzungumza na Wananchi Kijiji cha Tanangozi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ,SACP Allan Bukumbi akizungumza na Wananchi Kijiji cha Tanangozi wakati wa uzinduzi wa kituo cha Mafuta cha Villa Energies Tanangozi.
Dickson Nathan Lutevele (Villa) akizungumza na Wananchi Kijiji cha Tanangozi baada ya uzinduzi wa kituo cha kuuzia Mafuta cha Villa Energies Tanangozi.



Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP - Iringa.

WANANCHI  Mkoani Iringa  Wametakiwa kudumisha ulinzi ,amani na upendo kwa maslahi ya kila mmoja kwa itikadi yake ya Kidini na Kisiasa kwa maslahi ya Nchi.         


Hayo yamesemwa na Viongozi wa Serikali, Dini na Siasa wakati wa uzinduzi wa kituo cha kuuza mafuta cha kampuni ya Villa Energies Tanangozi Wilaya ya Iringa Vijijini.

                                              

Mgeni rasmi Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Iringa Ndugu Joseph Lyata,wakati akizindua kituo hicho cha Villa Energies alisema ni wakati sahihi kwa Wananchi na Wakazi wa Kata ya Mseke Tanangozi kutumia fursa hiyo ya Uwekezaji kwa manufaa ya Wananchi na si vinginevyo.


Ndg.Lyata alisema anapenda kumpongeza Ndg.Dickson Lutevele (Villa )kwa Uamuzi wake wa kufungua kituo hicho katika eneo ambalo litapelekea fursa kwa Wananchi na hasa wanaozunguka eneo la Tanangozi.                           


" Wananchi Tanangozi Muwekezaji ametekeleza kwa kuwekeza sasa ni jukumu letu Wananchi kuhakikisha ninyi ndio wanufaika Wakubwa kwa kupata ajira".                          


Hivyo uwepo wenu Tanangozi  suala la kulinda Usalama wa mali za Muwekezaji ni jukumu lenu na ninyi ndio mnatakiwa Walinzi namba moja .


" Mimi ni Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa kwa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi hivyo ninaamini Ndg.Villa ambaye ni Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Mufindi amewaletea fursa na hivyo hakikisheni mnaitumia vizuri Inawanufasha na sio mnaanza kuiba." Alisema Lyata.                       


Ndg.Lyata alisema pamoja na kumpongeza Ndg.Dicksin Lutevele (Villa) kwa Uamuzi wake wa kufungua kituo hicho bado anamshukuru kwa kutekeleza sera na Ilani ya CCM kwa kuongeza ajira kwa Wananchi na kuomba Wafanyabiashara wengine mkoani Iringa kuiga mfano wake.    


Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Iringa  Kamishna Msaidizi  Mwandamizi SACP Allan Bukumbi ,alisema anaamuni kuwa hakuna anayependa vitendo vya uhalifu na hivyo kuwataka Wananchi wa Tanangozi  na Mkoa mzima wa Iringa kujiepusha na vitendo hivyo.                                     


SACP Bukumbi aliwataka Wananchi kupinga vitendo vya Ukatili wa kijinsia na Uvunjifu wa haki za Binadamu kwa  kukemea na kutoa taarifa za Wahalifu kwa wakati.           


" Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wananchi na Wadau wengine wa Maendeleo Iringa tunahitaji amani na utulivu kwa kupambana na vitendo vya uhalifu "  aliongeza SACP Bukumbi.                    


  Hata hivyo alisema Jeshi la Polisi halitakuwa na huruma kwa mtu yeyote atakaye patikana akijihusisha na uhalifu ndani ya Mkoa kwani hatua kali za Kisheria zitachukuli ikiwa ni pamoja na kumkamata na kisha kumfikisha  Mahakamani kwa mjibu wa  Sheria.                             


"Toeni Ushirikiano wa  haraka kwa kutoa taarifa mapema   dhidi ya uhalifu wowote katika maeneo yenu ili kukabiliana na Wahalifu ili kuwafanya Wananchi waendelee na shughuli za maisha." Aliongeza kusema SACP Bukumbi.


Awali Mfanyabiashara huyo Ndg.Dickson Nathan Lutevele  (Villa) alisema anawashukuru Wananchi wa Tanangozi kwa kujitokeza kwa wingi katika hafla hiyo fupi na kusema atahakikisha anatoa Ushirikiano wa hali na mali kwa itakavyo mpendeza Mwenyezi Mungu.                                   


" Kwa upendo huu ambao Wana Tanangozi mmenionyesha Mimi na familia yangu nitahakikisha tunaunga mkono shughuli za Maendeleo na kijamii ili kubakiza fursa zote zinaifaisha Jamii inayotuzunguka." Alisema Villa.                         Katika hafla hiyo Ndg.Villa alimuahidi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa SACP Bukumbi, kuwa pindi kituo cha Polisi Kata kitakapo kamilika kampuni ya Villa Energies Tanangozi itatoa Pikipiki moja kwa ajili ya kuimarisha Ulinzi ndani ya Kata hiyo.                


Ndg.Villa aliongeza kuwa kampuni ya Villa Energies Tanangozi itahakikisha inasaidia kusomesha Watoto watano kuanzia sasa hadi mwisho wa kupata elimu yao wale wanaoishi katika Mazingira magumu na kati ya 20 waliopo kituo cha kuelekea Watoto Katika Kata hiyo,


Pamoja na kutoa ahadi ya Pikipiki kituo cha Polisi na kituo cha kuelekea Watoto wanaoishi katika Mazingira magumu,Ndg.Villa ameuomba Uongozi wa Serikali katika Kata hiyo kutafuta Vijana 30 ambao watapatiwa ajira katika Viwanda vyake vya kuchakata Mbao katika maeneo ya Mafinga na  Mgololo Wilayani Mufindi na Njombe mkoani Njombe.                                  


"Haya yote nayafanya ili kusaidia Jamii na Wananchi wa Tanangozi ambao wamewezesha na kuruhusu kituo hiki kujengwa hapa Tanangozi hivyo ni sehemu ya fadhira kwa Wananchi na Serikali.            


Upande wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Mseke Ndg.Villa alisema atatoa bendera za CCM kwa wajumbe na wenyeviti wa Matawi wa CCM wote pamoja na Mwenyekiti wa CCM Kata.                                     


"Wana Tanangozi na Mseke Mimi ni Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mufindi kama Katibu wa Siasa na Uenezi lakini kwa hapa Wilaya Iringa nakabidhi bendera za CCM kwa mapenzi ya Chama cha Mapinduzi CCM .".                                    


Mfanyabiashara Chesco Ng'umbi (CF) kwa niaba ya Wafanyabiashara wa Vituo vya Mafuta Mikoa ya Iringa na Njombe aliwaomba Wananchi hao kufanyakazi kwa uaminifu na kujiepusha na vitendo vya Wizi na udokozi Katia maeneo waliyopewa fursa ya kufanyakazi katika makampuni ya Villa.              


" Ndugu zangu fursa mmeipata. kwa Villa hivyo jiepusheni na kujihusisha na vitendo vya uhalifu zaidi saidieni kutoa taarifa za uhalifu badala ya kuingiza tamaa kwa Boss wenu." Alisema Mkurugenzi wa Makampuni ya CF".               


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI