Mbunge wa Buhigwe Felix Kavejuru akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi shule ya Sekondari Katundu wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Katundu katika halmashauri ya Buhigwe mkoani Kigoma wameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Raisi Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa shule mpya za sekondari ambazo zimewezesha kuondoa changamoto zilizokuwa zikiwakabili na kuimarisha taaluma.
Wanafunzi hayo wameeleza hayo mbele ya Mbunge wa jimbo la Buhiwe,Felix Kavejuru aliyetembelea shule hiyo na kuwa na kikao cha Pamoja na uongozi wa shule,wanafunzi, wazazi na viongozi mbalimbali.
Baadhi ya wanafunzi hao akiwemo Dada Mkuu wa shule hiyo, Mickness Bigilifodi na Kaka Mkuu Moabi Malaki walisema kuwa awali wakiwa shule ya Sekondari Nyamirambo Kijiji cha Kajana Zaidi ya kilometa 15 walikuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kulazimika kupanga nyumba ambazo zilikuwa zinasumbua inapofika wakati wa kulipa kodi.
Awali Mkuu wa shule hiyo, Gaston Tibaigana alisema kuwa shule mwaka 2021 serikali ilitoa kiasi cha shilingi 470 milioni ambazo ziliwezesha ujenzi wa madarasa manane, maabara tatu, jengo la utawala, maktaba moja, chumba cha Computer na matundu 20 ya vyoo akieleza shule kupata mafanikio makubwa ya kitaaluma licha ya muda mfupi tangu kuanzishwa kwake.
Akizungumza katika mkutano huo Mbunge wa jimbo la Buhigwe,Felix Kavejuru alisema kuwa amefanya jitihada kubwa kuisukuma serikali kuwezesha ujenzi wa shule hiyo kutoakana na kero kubwa ya wanafunzi kusafiri mrefu kufanya masomo kwenye shule hiyo na wengine kulazimika kupanga kwenye nyumba za watu huku wakiwa hawana uangalizi wowote.
Kavejuru alisema kuwa ujenzi wa shule hiyo pia ulipewa msukumo na Makamu wa Raisi, Dk.Philip Mpango na kwa sasa serikali imeshatoa pesa nyingine kiasi cha shilingi milioni 110 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya walimu ambayo itakuwa ya familia mbili
Mwisho.
0 Comments