Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), imetoa rai kwa wagombea kwenye uchaguzi unatarajiwa kufanyika hivi karibuni kuzingatia muongozo wa uchaguzi ili kuepuka kuondolewa kwenye kinyang'anyiro.
Hayo yameelezwa Julai 20, 2021 na Mjumbe wa Kamati hiyo Wakili, Francis Stolla kwa niaba ya Mwenyekiti wa kamati, wakati akizungumza katika ufunguzi wa mdahalo wa wagombea Urais wa Chama hicho, ambao umefanyika kwenye ukumbi uliopo kwenye ofisi kuu za chama hicho Jijini Dar es Salaam.
“Katika kipindi hiki kamati inaendelea kuratibu zoezi zima la uchaguzi mkuu katika ngazi zote ambazo zinagombewa. Na rai ya kamati ni kwamba wagombea wote wanapaswa kuzingatia mwongozo wa uchaguzi ambao ulitolewa na kamati ya uchaguzi mwaka 2023”amesema kuwa Wakili Francis Stolla
Ameongeza kuwa wagombea wanatakiwa kuzingatia mwongozo huo unaosisitiza matumizi ya lugha yenye rafiki, kuepuka uvunjifu wa amani na kuheshimiana pamoja na taratibu nyingine.
Amesema kuwa kamati hiyo inayo mamlaka ya kumuondoa mgombea atakaye kiuka muongozo huo, hivyo amewahasa kuwa makini kufuata utaratibu.
Aidha katika mdahalo huo hoja ambayo pia iligusiwa kwa ukubwa na wagombea ni kuhusu ushawishi wa TLS kuonekana kupungua ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.
Kutokana na hoja hiyo wagombea kwa namna tofauti wamekili suala hilo huku wakiweka wazi mikakati yao ambayo wanadai kuwa wakipewa ridhaa watarejesha utamaduni wa chama hicho unaodaiwa kuteteleka kwa siku za hivi karibuni.
Wagombea katika nafasi ya Urais wa TLS ni Wakili Revocatus Rubigili Kuuli, Wakili Emmanuel Augustino Muga, CAPT. Ibrahim Mbiu Bendera, Wakili Paul Revocatus Kaunda na Wakili Sweetbert Nkuba,
Pia wagombea Urais kwenye Chama cha Mawakili vijana (TYL) ni Wakili Emmanuel Phalet Ukashu na Wakili Denis Bwana ambao nao wamefanya mdahalo.
Uchaguzi wa Chama hicho unatarajiwa kufanyika August 2, 2024 jijini Dodoma.
0 Comments