Header Ads Widget

ABIRIA WAKWAMA TAZARA MAKAMBAKO

 


Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP Makambako.

ABIRIA wa Serikali la reli ya Uhuru ya Tanzania na Zambia (TAZARA) wamekwama kituo cha Makambako mkoani Njombe.                                  


Matukio Daima APP imejulishwa kuwa Jumla kuna treni mbili ambazo ilitakiwa zipishane hapo moja kutoka Mlimba ijulikayo kwa jina la Udzungwa maarufu treni ya daladala  ya Mwakyembe na Ile ya kutoka Mbeya kwenda Dar es salaam iitwayo Kilimanjaro.                          


Bw.Damasi Mlwale (35) ameiambia Matukio Daima APP kuwa alifika kutoka Kijiji cha Njoo mlole Njombe vijijini  Stesheni ya TAZARA Makambako majira ya saa 11:05 Alasri akiambiwa treni ya Kilimanjaro kutoka Mbeya itapita saa 2:00 kamili usiku .                         


Bw.Mlwale aliongeza kusema ilipofika saa 3 tangazo lilitoka la kuwataka abiria kuwa na subira kwani treni ya Mwakyembe imekwama Stesheni ya TAZARA Mlimba kufuatia barabara kupata hitrafu " "reli imetanuka" hivyo abiria wote waingie kwenye treni kubwa ya Kilimanjaro.                            


Alisema hapo ilibakia kimya abiria wa Kilimanjaro waliopandia Kituo cha Makambako walijikuta wakijazana kwenye treni moja na kukesha stesheni hadi asubuhi saa 3 ambapo treni ndogo ya daladala ya Mwakyembe iliingia.          


" Baada ya treni ya daladala ya kutoka Mlimba kuingia tukatangaziwa kuwa Injini (Locomotive) ya kutoka Mlimba inafungwa kwenye mabehewa ya treni ya Kilimanjaro kutoka Mbeya kwenda Dar hivyo abiria tuliopandia Makambako wote tunasafiri na treni kubwa na treni ndogo ya Udzungwa inabakia Makambako maana Locomotive yake inahitrafu " Alisema Bi.Mwanahawa Said.


Matukio Daima APP imejulishwa kuwa hadi saa 3 :30 Alasiri habari hii inatumwa abiria hawakuwa wanafahanu kinacho endelea na Utawala wakiulizwa na abiria hawakuwa tayari kuzungumza chochote.       


Matukio Daima APP inaendelea kuwasiliana na Steshani Master (DC) wa kituo kikuu cha Mlimba ili kufahamu hatima ya abiria hao .           



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI