Header Ads Widget

UHITAJI WA KATIBA MPYA, TUME HURU YA UCHAGUZI WATAJWA.

 


NA JOSEA SINKALA, MBEYA.


Vuguvugu la upatikanaji wa katiba mpya nchini Tanzania linaendelea kupamba moto baada ya jukwaa la katiba nchini kufanya kongamano na makundi mbalimbali jijini Mbeya na kuhamasisha wananchi kuendelea kupigania katiba mpya na bora kuhakikisha inapatikana sasa kama anavyoeleza Thobias Messanga, Mkuu wa Programu ya Jukwaa la Katiba nchini Tanzania.



Mwenyekiti wa jukwaa la katiba nchini Tanzania Dkt. Ananilea Nkya ni miongoni mwa wanenaji waliokuwepo kwenye kongamano hilo ambaye ameeleza umuhimu wa kupatikana kwa katiba mpya kuwa italeta uwajibikaji wa viongozi wa umma na kupunguza mamlaka ya mkuu wa nchi.



Dkt. Nkya amewataka wananchi kuwapuuza baadhi ya watu na wananchi wanaodai katiba mpya sio chakula wala maji ya kunywa kwa maelezo kuwa katiba ndio chanzo na msingi wa maendeleo ya mtu na Taifa pia.


Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya jukwaa la katiba nchini Tanzania Mwalimu Deus Kibamba, amesema rasimu ya jaji Joseph Warioba ilichukua maoni mbalimbali baada ya kukusanya maoni ya wananchi kuelekea kuandikwa kwa katiba mpya.



Mhadhiri huyo Deus Kibamba anasema katiba mpya ni jambo la kupiganiwa kuhakikisha inapakana licha ya kuwa tangu mwaka 1977 katiba ya mfumo wa mwingereza na kutumika na Tanzania imeendelea kufanyiwa marekebisho lakini bado sio katiba bora kwa sasa.


Baadhi ya wananchi kutoka makundi mbalimbali jijini Mbeya wameeleza kunufaika na kongamano hilo la katiba mpya na kutaka mabadiliko ya katiba ambayo itaweka usawa ambapo wameshauri mambo mbalimbali ikiwemo kupunguzwa kwa baraza la mawaziri, viongozi wa kuteuliwa wachaguliwe na wananchi wa eneo husika na Mawaziri kutokuwa wabunge.


Huu ni mwendelezo wa vuguvugu la upatikanaji wa katiba mpya nchini Tanzania kutokana na ukweli kwamba katiba ya sasa iliyotungwa mwaka 1977 na kufanyiwa marekebisho mara kadhaa imepitwa na wakati ikilinganishwa na mahitaji ya sasa juu ya sheria mama hiyo ambapo wananchi na taasisi mbalimbali nchini wanashinikiza kuandikwa kwa katiba mpya na bora itakayoendana na kipindi cha sasa na miaka mingine ya usoni.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI