Na, Matukio daima App, Iringa
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa imefanikiwa kuokoa Tsh Milioni 49 za mkopo kutoka mfuko wa maendeleo ya Vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya kazi, Vijana ajira na wenye ulemavu.
Fedha
hizi ziliombwa na mwananchi mmoja aliyedaiwa kuwa ni mkazi wa Mafinga kwa
kudhaminiwa na Halmashauri ya Mji wa Mafinga ambapo, baada ya TAKUKURU
kuingilia kati, ilibaini kuwa muombaji huyo hatambuliki kuwa ni mkazi wa
Halmashauri ya Mji wa Mafinga pamoja na aina ya biashara anayodai kuifanya
haifahamiki.
Aidha
TAKUKURU ilibani kuwa muombaji alikuwa ametengenezwa ili baada ya kupokea mkopo
huo atoroke na kuiachia Halmashauri ya Mji wa Mafinga deni hilo, hivyo muombaji
hakupewa mkopo na fedha hizo kuokolewa.
Katika
hatua nyingine, Takukuru mkoa wa Iringa, imefanikiwa kuokoa kiasi cha Shilingi
mililioni mbili (2,000,000) kutoka kwa Maafisa wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) Mkoa wa iringa.
Maafisa
hao walipokea fedha hizo kutoka kwa mfanya Biashara aliyekutwa akifanya
biashara bila ya kuwa na Mashine ya Kutoa Stakabadhi za kieletroniki(EFD).
Katika
kipindi cha mwezi April hadi June 2024 takukuru mkoa wa Iringa imefuatilia
utekelezaji wa miradi ya maeneleo 16 yenye thamani ya shilingi bilioni sit ana milioni
mia mbili katika sekta za maji, afya, elimu, usafirishaji na ujenzi ambapo
miradi mitatu iliyopo wilayani Mufindi, imekutwa na mapungufu naTakukuru imetoa
ushauri kwa wasimamizi wa miradi hiyo ambayo imefanyiwa kazi.
0 Comments