Header Ads Widget

SIMBA SC WATANGAZA RASMI UMMOJA WAO NA MTANDAO WA VODACOM







Na: Dickson Bisare Matukio Daima App -Dar Es salaam.


Timu ya Simba Sc wametangaza ummoja wao ambao hafla ambayo  imefanyika  leo katika ukumbi ya Kilimanjaro Hoteli jijini Dàr es salaam.


Akizungumza mbele ya vyombo vya  habari Afisa Habari wa timu ya Simba SC

Ndugu Ahmed Ally ameenza kwa kuelezea mafanikio ambayo wao kama timu wamepata tangu mtandao huo wa  Vodacom kuingià na kuifadhili Ligi kuu ya Tanzania.(Vodacóm Premier league) 


"Tunafahamu jitahada kubwa ambazo mmezifanya haswa kipindi mlikuwa wafadhíli Wakuu wa ligi kuu ya Tanzania (Vodacom Premier league) hakika hatuweza kuwasahau zaidi ya kuwàshukuru sàna Vodacom." Ahmed Ally Afisa Habari Simba SC.


Ameendelea mbele na kusema. "Huduma inapaswa mashabiki wa Simba tuishi kwa vitendo ili klabu ifikie malengo yake ya kuongeza kipato. Kuanzia sasa Wanasimba wote tunatumia Simba Mastori na Simba Bundle." Ahmed Ally.


Naye Afisa Masoko wà shirika la Vodacom Bi.Grace ameanza kwa kuogelea wào watakuwa na mchango gani haswa wakati huu àmbao wameingia ubia na timu ya simba Sc


"Sisi kama Vodacom tunatambua umuhimu wétu kuingia ubia huu na timu yà Simba Sc tunaenda kuhakikisha kwamba tunaenda kuitangaza timu Simba Kupitia simu katíkà mtandao wetu wa Vodacom ambayo inaenda kupatikana katika simu zote,smartphones na simu zingine ndogo (Viswàswadu)." Alisemà.


"Tumefurahi kujiunga na Simba tukiwa kama technology partner kuwawezesha Simba kuwafikia mashabiki wao.Tukiwa na wateja zaidi ya milioni 22 itawezesha mashabiki kupata huduma ya ujumbe na sauti kuhusu timu yao.Huduma hizo mbili itakuwa ni Simba Mastori na Simba Bundle,"  Bi.Grace ChambuaMkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Vodacom.


Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa wa timu ya Simba Sc ndugu Imani Kajula ameanza hotuba yake mbele ya vyombo vya Habari na  kusema.


"Vodacom wana wateja zaidi ya milioni 22, Simba tuna zaidi ya mashabiki 20, na wote ni rangi nyekundu. Nashukuru pia Vodacom mobile kuwekeza milioni 300 kwa maendeleo ya timu yetu ya vijana."


"Mashabiki mna wajibu wa kutumia huduma za klabu ili kusaidia  kuongeza mapato ya klabu. Simba Bundle itaanza kufanya kazi kesho asubuhi." Imani Kajula Mtendaji Mkuu wa Simba SC.


"Tunathamini sana mchango wetu katika klabu yetu. Wanachama na mashabiki wa Simba siku zote wamekuwa mbele kuunga mkono jitihada za klabu ili kusonga mbele hivyo nawasihi mkatumie huduma hii mpya ambayo tumewaletea."- Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu.


Huku hàyo yakiendelea naye Waziri mwenye dhàmàna ya Utamaduni,Sanàa na Michezo Mhe.Dkt Damas Ndumbaro ambaye àlikuwa mgeni rasmi katikà hafla hiyo ya kuingià ubià Kati ya Simba Sc nà Mtàndao wa Vodacom àmesema.



"Ni ngumu sana kunitenganisha mimi na Simba sababu ndio klabu niliyochagua kuishangilia. Na leo tumekutana hapa katika tukio hili kubwa la ushirikiano wa Simba na Vodacom."- Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro. 


"Ubunifu wa Simba na Vodacom sio jambo tu la kupongeza ni jambo la kuingwa. Ni jambo la kutupatia mashabiki, wanachama zaidi lakini pia rasilimali fedha. Mwekezaji namba moja ni shabiki."- Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.


"Ningeomba vilabu vingine vya ligi na championship vijifunze utawala bora kwa Simba. Takwimu zinaonyesha Simba ndio klabu kubwa Afrika Mashariki na Kati na inakutana na mtandao mkubwa wa Vodacom kufanya kazi."- Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI