NA WILLIUM PAUL, MWANGA.
MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ametoa agizo kwa wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri zote mkoani huko kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kudhibiti hoja za mdhibiti mkuu wa serikali badala la kuwaachia mweka hazina na Mkaguzi wa ndani pekee.
Babu alitoa agizo hilo jana wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo kujadili hoja tisa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30 mwaka 2023.
"Hawa sio wenye hoja peke yao, nyie wakuu wa idara na wakuu wa vitengo hili ni jukumu lenu wote, mkiwaachia peke yao hawatawezi kufanya hiyo kazi,naomba suala la hili lizikatiwe katika kumaliza au kupunguza hoja,"alisema
Alisema kwa kufanya hivyo ni kukabiliana na hoja ambazo huletea halimashauri doa huku akiwataka kuhakikisha mkaguzi wa Hesabu za Serikali anapata vitendea kazi ikiwemo mafuta ya gari kwa wakati na kwa haraka.
"Ila mnavyanzo vingi sana vya mapato, tunaomba mwendelee kuwa wabunifu na kuongeza bajeti"alisema RC Babu
Aidha Katibu tawala wa msaidizi wa mkoa, usimamizi ufuatiliaji na ukaguzi miradi Ponceano Kilumbi alizitaka kuongeza kasi ya ukusanyaji wa madeni hasa kwa mikopo ya wanawake, vijana na wa watu wenye ulemavu.
Mwisho
0 Comments