Header Ads Widget

POLISI YATOA KAULI KIGOGO WA TRA ALIYEKAMATWA NA MENO YA TEMBO

  


Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa Kigoma Iddi Kiyogomo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa Kaimu Meneja wa TRa wilaya Kibondo mkoa Kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo jumatatu wiki hii

Na Fadhili Abdallah,Kigoma


POLISI mkoani Kigoma imesema kuwa baada ya kumtia mbaroni Kaimu Meneja wa Mamlaka ya mapato (TRA) wilaya Kibondo mkoa Kigoma kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo upelelezi mkali unaendelea kubaini mtandao wa watu wengine wanaohusika na biashara hiyo kupitia kwa meneja huyo.

 

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Iddi Kiyogomo akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake mjini Kigoma alisema kuwa kwa sasa mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi wilayani Kakonko katika kituo kikuu cha wilaya wakati upelelezi wa shauri hilo ukiendelea.

 

Kaimu Kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma alisema kuwa hakuna mtu mwingine yeyote ambaye ameshakamatwa hadi sasa Zaidi ya Meneja huyo wa TRA wa wilaya ya Kibondo ambapo ametoa wito kwa watu wenye taarifa zidi kuhusu mtuhumiwa huyo kushirikiana na polisi katika upelelezi.

 

Licha ya jina la Mtuhumiwa huyo kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii nchini polisi imekataa kutaja jina la mtuhumiwa wala kutaja thamani ya meno hayo ya tembo kwa sasa ambayo ni mazima na hayajakatwa.

 

 Mtuhumiwa huyo alikamatwa mwanzoni mwa wiki hii katika kizuizi cha polisi cha Kihomoko wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma akiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili  STL 7274  ambayo iliwekwa   namba bandia yenye namba T 501 AGS akiwa safarini kutoka Kibondo mkoani Kigoma kuelekeamkoani Kagera.

 

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI