Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Njombe ambaye ni mkuu wa mkoa Antony Mtaka ameagiza kufanyika kwa Oparesheni maalumu itakayosaidia kubaini wahusika wa matukio ya mauaji yanayoendelea likiwemo la mfanyabiashara wa miamala ya fedha.
Mtaka ametoa agizo hilo wakati akizungumza na Askari Polisi huku akielekeza vyombo vyote vya usalama kuungana ili kubaini wauaji hao wanaorudisha nyuma maendeleo ya wananchi na kuwatia hofu wafanyabiashara.
Awali mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga ameagiza kutafutwa kwa wahalifu na wauaji hao ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amesema jitihada za kuwatafuta waliohusika na mauaji ya mfanyabiashara huyo zinaendelea huku akiwatoa hofu wananchi na kuwataka waendelee na Shughuli zao kama kawaida.
0 Comments