BENKI ya NMB Imewakutanisha Waalimu zaidi ya 200 wa halmashauri ya wilaya Nkasi katika kuadhimisha siku ya Waalimu ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo namna ya kuitumia mikopo wanayoipata katika kujiimarisha kiuchumi na kujipanga vyema namna ya kuishi baada ya kustaafu.
Akizungumza na Waalimu hao Kaimu meneja wa NMB kanda ya nyanda za juu kusini Daniel Zake amesema kuwa wao kama Benki wameiandaa siku hii ya Mwalimu spesho kama hatua ya kutambua mchango wa Walimu kama Moja ya kundi linalopata huduma za za Benki hiyo na kuwa na mchango mkubwa katika Benki hiyo.
Amesema kuwa Moja ya huduma kubwa ni ya mikopo na kuwa wao kama Benki wameamua kukutana nao Ili kuwajengea uwezo namna ya kuitumia mikopo wanayoipata Ili iweze kuwanufaisha na kujiandaa katika maisha ya baadae hasa baada ya kustaafu badala ya kuendelea kuwapatia mikopo Bila ya kuwa na elimu namna njema ya Matumizi ya fedha hizo
Amefafanua kuwa Benki hiyo inatamani kuona maisha ya Walimu yanakua endelevu hata baada ya kustaafu Bila ya kuwa na wasiwasi wa kimaisha au kuyumba kiuchumi na kuwa suluhisho pekee kwao ni kukopa na kuiendeleza mikopo hiyo Kwa kuzifanyia kazi zenye tija hasa uzalishaji utakaowawezesha hata kujiwekea hakiba wenyewe kama maandalizi ya kuelekea kustaafu katika program Yao ya jiwekee.
Meneja wa NMB tawi la Nkasi Josephine Fute Kwa upande wake amedai kuwa kwa sasa NMB wanayo Programme maalumu iitwayo "Jiwekee" na katika siku hii muhimu ya Mwalimu Spesho watafundishwa namna njema ya kujiwekea hakiba ambayo itakua na msaada mkubwa baada ya kustaafu badala ya kutegemea kiinua mgongo pekee kinachotolewa na serikali.
" Programme hii ya jiwekee ni Moja ya huduma ambazo Benki imeona kwamba inaweza kuwasaidia watumishi wa Umma hasa Waalimu kujiwekea hakiba wenyewe na kujikuta wakati wa kustaafu anakua na hakiba ya kutosha hasa Ile aliyojiwekea yeye mwenyewe na Ile ya mwajili na kujikuta wanaishi maisha yasiyo kuwa na wasiwasi wowote wa kimaisha"
alisemawatawafundisha namna ya kupata mikopo mingine ikiwemo Ile ya kilimo,Uvuvi,Biashara na mengineyo mengi ambayo itawasaidia kuwa wajasiliamali Kwa kuwa na shughuli nyingine za kiuchumi nje ajira zao za Ualimu na kuwa Hilo linawezekana Kwa maana wamefanya utafiti wa kutosha na kujikuta wanaweza kuishi maisha mazuri zaidi katika siku za usoni.
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Vicent Magendela amesema Watumishi wengi wakiwemo Waalimu wamekua waathirika wakubwa Kwa kukosa elimu ya Matumizi ya fedha hasa pale wanapopata fedha Kwa wingi baada ya kustaafu na kuwa elimu hiyo itawasaidia kuwa na uzoefu wa kumiliki fedha nyingi toka wakiwa kazini na hata wakistaafu hakuna kitakachowachanganya.
Na aliitumia fursa hiyo kuwataka Waalimu hao kuendelea kujifunza namna ya kutumia huduma hizo za Kibenki lakini na kufanya shughuli zao katika muda wa ziada Ili hata baada ya kustaafu wasiwe wageni katika maisha mapya watakayokwenda kuyaishi.
Walimu Kwa upande wao wamekiri kuishi maisha magumu baada ya kustaafu hasa baada ya kushindwa kuzitumia fedha nyingi zinazopatikana Kwa mpigo ikiwa ni pamoja na kuandamwa na madeni mengi hasa Kwa kukopa katika maeneo mbalimbali na kuwa sasa watakwenda kuwa mabalozi Kwa Walimu wenzao namna ya kujiwekeza na kuzitumia huduma mbalimbali za Kibenki.
Janeth Maliago,Christina Bwataye na Michael Joachim wameishukuru Benki ya NMB Kwa Progromme hiyo na kutambua changamoto wanazozipitia na kuwa sasa ni muhimu wakaendelea kuzoea kumiliki fedha na kuwa na mzunguko mkubwa kitakachowafanya wao kutoona kile kilichopo mbele Yao kuwa ni jipya
Benki ya NMB imekuwa na Utaratibu wa kukutana na Walimu na kuwajengea uwezo namna njema ya kuishi na kuepukana na mikopo umiza kutoka Kwa wakopeshaji binafsi ambao ni matapeli
0 Comments