Na fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar
Bodi ya Sukari nchini Tanzania ( SBT) imesema tangu walivyo binafsisha viwanda hadi sasa uzalishaji wa sukari bado haujatosheleza mahitaji ya watumiaji nchini humo, kwani walikua wakitumia wafanyabishara kuingiza sukari.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Prof Kenneth Bengesi amesema kuwa miaka ya nyuma walikua wakitumia wafanyabiashara kwa ajili ya kuziba pengo la sukari nchini.
"Mfumo uliokuwa ukitumika miaka ya nyuma kuingiza sukari ili kuziba pengo tulikuwa tukitumia wafanyabiashara, lakini kwa sababu ilionekana sukari iliyokuwa ikiingia nchini ilikuwa ni kiasi kikubwa ambacho kilikuwa kikivuruga utulivu wa soko la ndani, Ilipofika mwaka 2015 Serikali ilichukua jukumu la kufanya mabadiliko ya kanuni za sheria ya sukari za mwaka 2010 na kubadilisha mfumo wa uingizaji wa sukari"amesema Prof Kenneth
Aidha, amesema kuwa msimamo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuwalinda wananchi, wakulima, wawekezaji na wadau wengine muhimu kwenye sekta hiyo kwa kuhakikisha inafanya maboresho makubwa kwa maslahi ya Watanzanaia wote.
Amesema kuwa, wataendeleza majadiliano na wadau ili kutatua changamoto zote sambamba na kuikuza sekta ya sukari kwa sababu ni jambo nyeti na muhimu, hivyo wanalichukulia hili kwa umakini.
Hata hivyo, amesema kwa siku za karibuni kumekuwa na mijadala kadhaa kutokana na siku chache zilizopita kugubikwa na uhaba wa sukari hali iliyoibua hofu kwa watanzania wote.
0 Comments