Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP MUFINDI.
CHAMA CHA MAPINDUZI CCM Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa chini ya Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya,kinaendelea na kuwapiga msasa Wanachama wake ngazi za chini.
Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Mufindi Ndugu Dickison Lutevele (Villa ) awali anaendelea kuendesha Semina ya Uongozi ambayo inahusisha Mabalozi , Viongozi na Makada wa CCM katika ngazi zote za Kata.
Ndugu Dickison Lutevele (Villa) alisema Semina hiyo iliyopewa jina la " "TUNAZIMA ZOTE TUNAWASHA YA KIJANI" ni salaam kwa Wengine wasiopenda kwenda kwa mwendo kasi na miradi ya Maendeleo .
Awali mkutano wa ndani uliofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Sadani Ndugu Villa aliwataka Viongozi kuwa na Upendo na kupendana kikweli bila kufanyiana fitina kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu 2024.
" Mimi kama Katibu Siasa na Uenezi Wilaya ya Mufindi sitapeda kusikia eti fulani hajui kusoma na kuandika au ni mchawi na mshirikina Ili hali ni uzushu".
Alisema kuelekea Chaguzi mbali mbali kumekuwa na tabia za kuzushiana maneno ya uongo na fitina ili kuharibiana,Jambo hilo ni baya sana na hata Mungu hapendi.
"Inakuwaje Mtia nia na Mgombea aonekane ni mchawi, mshirikina na mlevi ! Kama sio fitina ni nini ?
Ndugu Villa akiendesha Semina na mafunzo ya Uongozi ndani ya Ukumbi wa Shule ya Sekondari Sadani ,aliwataka Wana CCM Wilaya ya Mufindi kuacha tabia ya kuwatenga Viongozi Wastaafu na Wazee kwani wanapaswa kushirikishwa kwenye Ujenzi wa Chama.
" Uongozi ni kupokezana kijiti haaiwezekani eti Kiongozi amestaafu au kura hazikutosha halafu wewe unachaguliwa unaanza kufurahia na kuanza kumkomoa kwa kusema safari "Chali" na humshirikishi kwenye shughuli za Chama hii haikubaliki! Alisema Villa.
Viongozi watahadharishwa kukumbushwa kuwa na wao waliopo Madarakani leo ndio Wastaafu wa kesho, hivyo Wasiwatenge wenzao katika kazi za Ujenzi wa Chama maana nao ni Wana CCM.
" Wana CCM Wilaya ya Mufindi kwa sasa sisi ni kuhamasisha Wananchi kujiandikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu 2024 na si vinginevyo na tunaendelea hadi mwakani 2025 Uchaguzi Mkuu na Kauli mbiu yetu " TUNAZIMA ZOTE TUNAWASHA MOJA YA KIJANI" na MH.DKT.Samia Suluhu Hassan .
Aidha akiwahutubia Wanachama na Wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Sadani , Ndugu Villa aliwataka Wananchi kushiriki kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu 2024 ikiwa na kumshukuru MH.Dkt.Samia kwa Miradi ya Maendeleo kwa Wananchi .
Alisema anampongeza MH,Dkt.Samia kuleta Ruzuku ya Mbolea na kufika kwa Pembejeo hizo za Kilimo kwa Wananchi na Miradi ya Maendeleo kwa Wananchi ya Afya ,Maji na Elimu.
Upande wao Waheshimiwa Madiwani wa Kata za Igombavanu na Sadani kwa niaba ya Wananchi wa Kata tatu za Sadani, Ikweha na Igombavanu walimshukuru Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Mufindi kwa kuwa kupiga msasa wa Kisiasa na kumuahidi kuyazingatia mafundisho yake.
Mh. Veronica Kilongumtwa Diwani wa Kata ya Igombavanu alimshukuru MH Dkt Samia kwa kuwajali na kuwaletea Miradi ya Maendeleo na miradi inatumika kwa kuwahudumia Wananchi.
Mh.Issa Idd Manga Diwani wa Kata ya Sadani mahali palipofanyikia Mkutano wa hadhara alisema fedha zote za Miradi katika Tarafa yote ya Sadani katika Kata tatu zimetumika kwa asilimia 💯 pasi na kupotea hata mia .
Hongera Mama mitano tena 2025/2030 , sisi Mufindi tunasema ! "TUNAZIMA ZOTE TUNAWASHA MOJA YA KIJANI " Kazi imekwisha " KAZI IENDELEE "
0 Comments