WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dkt SELEMAN JAFO ametoa wito Kwa Halmashauri zote Nchini kuhakikisha zinanunua dawa za Viuadudu Ili kuweza Kuuwa mazalia ya Mbu wa malaria ili kuondokana na kutumia Fedha Nyingi Ili kuweza kununua Dawa za kutibu ugonjwa wa malaria.
Wito huo ameutoa Wakati wa Ziara yake alipotembelea kiwanda Cha Viuadudu kilichopo Kibaha ambacho kinatengeneza Dawa ya kuua mazalia ya Mbu.
Aidha Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo NDC Nicolaus Shombe ameeleza malengo ya kuanzishwa Kwa kiwanda hicho.
Katika Ziara hiyo Waziri akiwa Wilaya ya Kibaha ametembelea kiwanda Eneo la kamaka industrial ambalo litajengwa Viwanda miasita na baadae Eneo la Viwanda la Sinno Tan ambalo litajengwa Viwanda Miambili.
0 Comments