Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Nape Nnauye akiwa kwenye mnara wa airtel kijiji cha Kumbanga ambapo alizindua mawasiliano ya mnara huo uliojengwa kupitia mpango wa Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) katika maeneo ya vijijini yasiyo na mvuto kibiashara
Na Fadhili Abdallah, Kigoma
Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Nape Nnauye amesema kuwa wananchi milioni 8.5 watanufaika na kuunganishwa kwenye mawasiliano ya simu za mkononi na vifaa vingine vya mawasiliano kupitia mpango wa uwekwaji minara 758 sehemu zisizo na mvuto kibiashara kupitia Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF)
Nape alisema hayo akianza ziara ya mikoa mitano ya kuzindua minara ya mawasiliano ambapo alifanya kazi ya kuzindua minara miwili katika wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma ambapo alisema kuwa ujenzi wa minara
ukaleta tija katika upatikanaji wa huduma na kuchochea maendeleo kwenye maeneo yao vijijini.
Hata hivyo Waziri huyo wa habari amewataka wazazi kuwaonya na kuwasimamia watoto wao ambao wamekuwa wakitumia vibaya uwekwaji wa minara hiyo ya mawasiliano kuzua taharuki, kuwatukana viongozi na kuharibu taswira ya nchi na viongozi.
Awali Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba alisema kuwa serikali imetenga fedha kwa ajili ya uwekaji wa minara 758 maeneo ya vijijini ambayo hayana mvuto wa kibiashara kwa makampuni na kufikia Juni mwaka huu tayari minara ya mawasiliano imewashwa na inafanya kazi.
Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja wa kanda ya Magharibi airtel, Isack Kijuu alisema kuwa uzinduzi wa mnara huo unaifanya taasisi hiyo kufikisha minara 86 ambayo imewashwa na airtel katika mpango huo chini ya UCSAF.
Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bunyambo wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wakati akizindua mnara wa mawasiliano wa kampuni ya halotel uliojengwa kupitia mpango wa mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF).
0 Comments