Dickison Nathan Lutevele (Villa) Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Mufindi, Wakati akizungumza na Wasanii Wilaya.
Na Fredrick Siwale - Matukio Daima APP - Mufindi.
CHAMA CHA MAPINDUZI( CCM) Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imewapashavu Wasanii wote wa Wilaya hiyo kwa kufungua milango na kuwakutanisha pamoja katika kufahamiana.
Tukio hilo limefanyika Julai 15 mwaka huu 2024 kwa Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Mufindi Bw.Dickison Lutevele (Villa) wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa CCM Mufindi.
Bw.Villa alisema lengo la kuwaita na kukutana na Wana tasnia hao ni kufahamiana na kushirikiana nao katika majukumu na kazi zao za Kisanii ndani ya Wilaya ya Mufindi.
Katibu Siasa na Uenezi Wilaya ya Mufindi akiwa na Katibu Siasa na Uenezi Kata ya Boma.
Alisema Wasanii ni tasnia ambayo ikitumika vizuri ni nyenzo sahihi ya kufikisha ujumbe kwa Wananchi kwa haraka zaidi tofauti na ilivyo sasa ambapo kuna tasnia ilioonekana kusahaulika.
" Nimewaita hapa ninyi Wasanii lengo likiwa ni kufahamiana na kufanyakazi kwa Ushirikiano na kuifikishia taarifa Jamii kwa njia rahisi kupitia Habari na Sanaa" Alisema Villa.
Katika mkutano huo Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya Bw.Villa kwa kushirikiana na Katibu wa Siasa na Uenezi Kata ya Boma Bw.Gift Mwachang'a ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Mpira wa miguu Wilaya ya Mufindi ,waliwataka Wasanii kushirikiana.
" Mimi kama Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Mufindi ninataka kuwahakikishia kuwa nitakuwa bega kwa bega na hatua kwa hatua kuwa Jamii na Wananchi wanapata taarifa na habari sahihi kutoka kwenye vyanzo sahihi." Alisema Villa.
Alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya inayoongozwa na Rais Mh.Dr.Samia Suluhu Hassan ,imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya shughuli za Miradi ya Maendeleo lakini Wananchi baadhi yao wanakosa kuwa na taarifa sahihi za Miradi .
" Kuanzia sasa Wasanii nitawatumia kwa Sanaa yenu na nitawashirikisha Waandishi wa habari Ili kuburudisha , kuhamasisha na kutangaza kuhusu shughuli mbali mbali za Maendeleo kwa Wananchi." Aliongeza kusema.
Pamoja na kuwakutanisha Wasanii hao aliwataka kuhakikisha wanafanya sanaa yao kwa kuzingatia kanuni, Sheria na Maadili ya Kitanzania ili kujenga Jamii yenye staha na Utamaduni halisi na sio kuiga tamaduni za Kigeni.
Upande wake Afisa Utamaduni wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw.Cleopa Josephat Shubi aliwataka Wasanii hao kuacha kufanyakazi zao bila kufuata taratibu na kanuni zake katika kufanya Sanaa kwa kufuata Sheria za Nchi zilizopo.
B.Shubi alisema ofisi iko wazi itumike na kushauri Wasanii kufika na kuzungumza iikiwa ni pamoja na kueleza changamoto wanazokabiliana nazo, ambazo ni ndani ya Sanaa na nje ya Sanaa kijamii na Kiuchumi.
Wasanii upande wao Wasanii Rustica Dalu na Bashil Mwagala walidai kuwa hawakuwa wanatambua hatua za kupitia hadi kufikia usajili.
"Kwa kutokufahamu tulikuta tukipitia changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na namna ya kupata usajili wa ndani wa msanii mmoja mmoja na ule wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) ." Alisema Mwagala - Katibu wa Chama cha Wasanii Wilaya ya Mufindi.
Bi.Rustica Dalu kwa upande wake alisema Mufindi wamechelewa sana kuwa wamoja kwa kuwa hawakuwa na Kiongozi ambaye alijitokeza kuwasaidia na kuwaongoza kitu cha kufanya ili kufikia mafanikio.
" Niombe Wasanii tushikwe mkono na Serikali ili kutufanikishia Sanaa na kutujengea uwezo kielimu na Kiuchumi kupitia raslimali zilizopo kama majengo ya CCM na Serikali ili yatumike kunyia mazoezi" Alisema Bi.Dalu.
Aidha Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya pamoja na kuwakutanisha Wasanii hao pia alikutana na Wazee na kutoe elimu kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuwataka Washiriki kujiandikisha na kugombea wakati utakapowadia.
0 Comments