Header Ads Widget

MHANDISI MAHUNDI ACHANGIA TSH MILIONI 23 UMOJA WA WANAWAKE

  




Na  Matukio Daima Media , Mbeya 


NAIBU Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi ameahidi kuchangia Mil 23  kwa ajili ya miradi ya  umoja wa wanawake.


Awali Mbunge huyo alichangia Mil.11 lengo likiwa ni kuendelea kusaidia uimarishaji wa miradi ya wanawake iliyopo mkoani Mbeya .


Amesema hayo wakati akizungumza na wanawake wa Wilaya ya Mbeya ikiwa ni mwendelezo wake wa ziara yake ya kuzungumza na wanawake pamoja kuwezesha miradi ya kiuchumi umoja wa wanawake mkoa wa Mbeya.


Aidha katika hatua  nyingine Mhandisi Mahundi ametoa simu mbili na kadi 1000  kwa ajili ya usajili wa wanachama pia amewataka Wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali zaidi akiwataka Wanawake kushikamana ili kumvusha Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa amefanya mambo mengi ukiwemo ujenzi wa shule, zahanati na miundombinu.


"Ndugu zangu wanawake mshikamane pamoja ili tuweze kumvusha Rais Samia kwani amefanya mambo makubwa mengi na ya msingi shime shime  tumpambanie mwanamke huyu ni shujaa "amesema Mhandisi Mahundi.



Mbali ya ahadi hizo Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewapatia vitenge kwa ajili ya sare  za huku akiahidi kukarabati ofisi ya Katibu.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI