Header Ads Widget

MBUNGE PROF. NDAKIDEMI AGAWA MICHE BORA YA MIGOMBA KATA YA KIBOSHO MASHARIKI.

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 


MBUNGE wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ameendelea na ziara zake katika Jimbo lake kwa kutembelea Kata ya Kibosho Mashariki ambapo aliongea na wananchi na kuwagawia miche bora ya migomba kwa lengo la kuboresha kilimo cha zao hilo katika Jimbo lake. 



Katika ziara hiyo Mbunge  aliambatana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali katika ngazi za Kata na Wilaya. 



Mbunge ameyafanya hayo alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Sungu ambapo walihudhuria mamia ya wananchi kutoka katika Vijiji vya Mweka, Sungu na Singa, akiwemo Paroko wa Parokia Teule ya Mweka, Padri Peter Asantebwana. 



Katika mkutano wake, Mbunge alitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha miaka minne ambapo Kata ya Kibosho Mashariki imeshapatiwa miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 4.778.



Kutokana na mafanikio haya makubwa, Mbunge amewaomba wananchi wote wa Kata ya Kibosho Mashariki kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan. 



Akiongea katika mkutano huo, Katibu wa CCM Wilaya, Ramadhani Mahanyu aliwaasa wananchi wa Kibosho Mashariki kuendelea kuunga mkono Serikali yao. 


Aliwashauri vijana kujiepusha na vitendo vya ulevi na washiriki kikamilifu kwenye miradi mbalimbali ya ujenzi wa Taifa lao.


Diwani wa Kata ya Kibosho Mashariki, Christopher Ndakidemi alifurahishwa na kufarijika na ugeni wa Mbunge na viongozi alioambatana nao, kwani wamejibu maswali mengi aliyokuwa akiulizwa na wananchi wa Kata hiyo.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI