Header Ads Widget

MBUNGE MBEYA VIJIJINI AKAGUA MRADI WA MAKAZI YA WALIMU

 


NA JOSEA SINKALA, MBEYA.


Mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Manasse Njeza, amekagua nyumba ya walimu wawili wa shule ya msingi Shitete kata ya Isuto ambayo imejengwa kwa thamani ya shilingi million hamsini.


Mbunge Oran Njeza ametembelea mradi wa nyumba moja itakayotumiwa na familia mbili (Two in one) ambapo Serikali ilitoa fedha shilingi million hamsini huku wananchi nao wakichangia nguvu kazi yao yenye thamani ya zaidi ya shilingi million moja.


Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Shitete Deogratius Sanga, amesema ukamilikaji wa nyumba hiyo ambayo bado vyoo vya nje pekee utasaidia watumishi kukaa maeneo ya shuleni ili kuboresha ufaulu shuleni hapo.



Mwalimu Sanga ameishukuru Serikali kujenga nyumba hiyo ya kisasa pamoja na Mbunge Oran Njeza kwenda kutembelea shule yake ili kuona mazingira ya utolewaji elimu kwa watoto na kuahidi kuendelea kuiunga mkono shule hiyo ikiwemo kuhakikisha chakula cha mchana kinapatikana kwa watoto wa shule.


Mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Njeza, amewataka wananchi na watumishi kuendelea kushirikiana ili kutoa elimu bora kwa mstakabali bora wa watoto kupata elimu ambayo ni urithi wa kweli.



Pamoja na kukagua nyumba hiyo ya watumishi, Mbunge Oran Njeza ametembelea na kukagua vyumba vya madarasa kisha kuzungumza na wanafunzi akiwasisitiza kuendelea kusoma kwa bidii na kuendelea kuahidi kuwa kila mwanafunzi wa darasa la saba atakayepata ufaulu wa alama A atapewa zawadi ya shilingi laki moja.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI