Header Ads Widget

KUMBUKUMBU YA SIKU YA MASHUJAA TANZANIA





Halmashauri ya wilaya ya Nkasi imeazimisha siku ya mashujaa kwa kufanya usafi maeneo mbalimbali ya mji wa namanyere ikiwemo soko la sabasaba,stendi ya mabasi pamoja na vutuo vya kutolea huduma za afya.


Leo ni siku ya kuwakumbuka na kuwaenzi mashujaa wetu, ambao kwa ujasiri na uzalendo wao, walijitolea maisha yao kwa ajili ya taifa letu. Tarehe 25 Julai ya kila mwaka ni siku maalum katika historia ya Tanzania, tunapotafakari mchango mkubwa wa mashujaa wetu katika harakati za kupigania uhuru na kuilinda nchi yetu.


Tunapoadhimisha siku hii, tunatambua na kuthamini juhudi zao katika kuleta amani, uhuru, na maendeleo kwa taifa letu. Ni wakati wa kukumbuka shujaa mmoja mmoja na kujivunia urithi wao wa ushujaa na uzalendo.


Tutafakari na Kujifunza


Siku ya Mashujaa inatupa fursa ya kujifunza kutokana na  historia yetu na kufahamu umuhimu wa kuwa na moyo wa kujitolea kwa ajili ya wengine. Tuwaenzi mashujaa wetu kwa matendo yetu ya kila siku, kwa kufanya kazi kwa bidii, kuilinda amani, na kushirikiana kwa maendeleo ya taifa letu.


Tushirikiane kwa pamoja katika kuendeleza na kulinda urithi huu wa mashujaa wetu, na kuhakikisha kuwa vizazi vijavyo vinaishi katika taifa lenye amani na ustawi.


Tunawatakia watanzania wote kumbukizi njema ya Siku ya Mashujaa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI