Header Ads Widget

JWTZ KUADHIMISHA MIAKA 60 YA KUANZISHWA KWAKE KWA KUFANYA ZOEZI LA KIVITA

 


Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar 


Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) linatarajia kufanya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwake Kwa kufanya zoezi kubwa la kivita ambalo halijawai kutokea tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo  likishirikisha kamandi zote za Jeshi.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Msemaji wa Jeshi la hilo Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda amesema kuwa kuelekea kilele cha maadhimisho hayo yatashirikisha kamandi ya nchi kavu, Baharini na Angani pamoja na vikosi maalum ambavyo vipo chini ya Mkuu wa majeshi.



Aidha amesema kuwa, zoezi hilo litafanyika katika  Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani, Tanga na Morogoro ambapo wananchi watashuhudia mapigo makubwa ya ardhini na angani, hivyo wanachi watakapoona hali hiyo wasiogope ni sehemu ya maadhimisho ya kilele hicho ambacho kinatarajiwa kuhitimishwa Septemba 23, mwaka huu.


Ameongeza kuwa, maandalizi yamekamilika na yamefanyika kwa maelekezo ya Mkuu wa Majeshi na yatasimamiwa na Kamandi ya nchi Kavu na Meja Fadhili Omar Nondo ambae atasaidiwa na Kamandi ya anga.


Sambamba na zoezi hilo la kivita pia kutakuwa na mambo mbalimbali ikiwemo mashindano ya utamaduni ya Mkuu wa Majeshi ambayo yanafanyika Kwa mara ya kwanza lengo likiwa ni kudumisha utamaduni wa kitanzania pamoja na michezo mbalimbali ambayo yanepewa Jina la CDF Cup.


Aidha, amesema kuwa kutakua na kituo cha kutoa huduma kwa wananchi pamoja na kutoa matibabu bure katika hospital zote za kanda za jeshi ambazo ni Kanda ya Arusha, Mwanza, Mbeya , Tabora pamoja na Zanzibar sambamba na vituo vingine maeneo ya Mbagala Dara es Salaam, Songea na Pemba.


Ameongeza kuwa shughuli  zote hizo zitahitimishwa na gwaride litakalokua na sura ya miaka 60 ambapo pia watakuwa na maonyesho ya kuonyesha wametoka wapi, wapo wapi na wanatarajia kuelekea wapi kwenye suala la Ulinzi na Usalama wa nchi.

.

Hata hivyo amesema  pamoja na maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ pia kutakuwa na maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano wa waasisi wa Taifa la Tanzania na China na ushirikiano wa kindugu wa miaka 60 wa mataifa hayo mawili.


Katika hatua nyingine Kanali Ilonda amesema Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana Jeshi la Ukombozi wa watu wa China katika maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa ushirikiano wa Majeshi hayo watafanya mazoezi ya pamoja  Julai 29 na kuhitimishwa Agosti 11 mwaka huu ambapo yatafanyika Mkoani Pwani na Dar es Salaam.


Amesema kuwa, zoezi hilo litagawanyika sehemu mbili ikiwemo zoezi la baharini na zoezi la nchi kavu Kwa kutumia vifaa na zana za nchi kavu na watashiriki  maafisa mbalimbali na wapiganaji,  na kutumia vifaa mbalimbali ikiwemo magari, ndege, na meli na zoezi hilo litafanyika kwa uwazi na wananchi wote wataona .


Ameongeza kuwa , ujio wa wageni hao kupitia zoezi hilo  itakua ni fursa kubwa kuweza kulitangaza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na kuitangaza Tanzania kwa vivutio mbalimbali vya kiutalii vilivyopo nchini .


Hata hivyo amesema Julai 16, meli ya madaktari itatia nanga katika bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu bure hivyo wananchi watumie fursa hiyo kupata matibabu na kufanya utalii ndani ya maji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI