Header Ads Widget

DC SAME AIBUKIA KWA WAFANYABIASHARA HEDARU.



NA WILLIUM PAUL, SAME. 


MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amefanya ziara ya kustukiza kwa wafanya biashara wa Hedaru yenye lengo la kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo za kikodi pamoja na kupokea mapendekezo yao kwa Serikali ili yaweze kutatuliwa kuwezesha gurudumu la maendeleo ya Wilaya hiyo kusonga kwa kasi. 


Aidha pamoja na kusikiliza kero na kupokea mapendekezo hayo lakini pia ziara hiyo inalenga kufuatilia utekelezaji wa Maagizo aliyoyatoa kwenye kikao cha kujadili mwenendo wa ukusanyaji wa mapato Wilayani humo kuhakikisha malengo waliojiwekea taasisi zote zinazokusanya mapato yanafikiwa kwa kutatua kero na changamoto zinazowakabili walipa kodi na kujenga mahusiano mema kati ya walipa kodi hao na taasisi hizo za Serikali zinazokusanya mapato.


“Sote tunafahamu Taifa lolote lile ulimwenguni ili liweze kukua kichumi na kuwahudumia wananchi wake vizuri lazima walipa kodi watimize wajibu wao wa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria ikiwemo ya ongezeko la thamani yaani (VAT), hivyo nimemuagiza Meneja wa (TRA) Same kuona namna ya kukutana na wanyabiashara wote kuwapatia elimu sahihi kuhusu kodi ya (VAT) kuwezesha kuwa na uelewa wa pamoja utakao saidia kuondoa usumbufu usio walazima utakaoweza kujitokeza wakati maafisa wanapopita kutekeleza majukumu yao ya msingi kisheria”, Alisema Kasilda.


Pia amezipongeza taasisi hizo kwa utekelezaji wa maagizo yake kikamilifu, pamoja na kuwashukuru wafanyabiashara wote na walipa kodi wengine Wilayani Same kwa kuendelea kushirikiana vyema na Serikali pamoja utii kwa mamlaka zilizopo kwa mujibu wa sheria, nakusisitiza ushirikiano huo uendelee kudumu ikiwemo kulipa kodi kwa wakati kuwezesha uchumi wa Wilaya kukua kwa kasi.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI