Basi la kampuni ya MUMUK kutoka Wilaya ya Mpanda Katavi kwenda Jijini Arusha imepata ajali Wilaya ya Igunga kuelekea Nzega na kusababisha Madhara kwa abiria.
Matukio Daima APP imeambiwa na shuhuda wa ajali hiyo kuwa basi hilo la MUMUK Dereva alikuwa akijaribu kulipita gari dogo la abiria aina ya Hiace na kugoligonga kwa mbele na kusababisha madhara kwa abiria wa kwenye Hiace.
Matukio Daima APP inaendelea kufuatia kwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ili aweze kuthibitisha idadi ya Wahanga wa ajali hiyo na chanzo chake.
0 Comments