Ajali basi la kampuni ya Zube trans limepinduka asubuhi katika eneo la Njirli Itigi Mkoani Singida.
Taarifa za awali zilizoifikia Matukio Daima APP ni kwamba gari limepata ajali eneo la Njirlii Itigi Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida na kusababisha Watu 28 kujeruhiwa.
Kwa mjibu ya shuhuda wa ajali hiyo alimeiambia Matukio Daima APP kuwa gari hilo lilikuwa likitokea Jijini Dar es salaam kwenda mkoani Mwanza na kupinduka katika eneo hilo.
Mganga Mkuu wa hospitali ya Manyoni ,Dr.Furaha Mwakafwila amesema wamepokelewa majeruhi 28,kati yao Wanawake 15 na Wanaume 13 huku wanne kati yao wakipewa rufaa kwenda Hospitali ya rufaa ya Mtakatifu Gasper Itigi na kwamba majeruhi wengine wanaendelea na matibabu .
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ,Mh.Kemilembe Lwota amesema tayari wamefanya mawasiliano na ndugu wa majeruhi hao wote kwa ujumla wao .
Aidha Mh. Kemilembe amesema baada ya kupata taarifa za ajali hiyo Jeshi la Polisi na Kambi ya Jeshi ya Mokiwa kwa kushirikiana na Wananchi walifika haraka na kutoa msaada kwa haraka ,ambao ulisaidia kutotokea madhara na maafa kwa abiria.
Ameiambia Matukio Daima APP kuwa taarifa ya kutoka kwa Wauguzi inasubiriwa kuhusu majeruhi watakaoruhusiwa ,ili wafanye utaratibu wa kuwawezesha kuendelea safari zao.
" Hawa ni ndugu zetu kama Serikali tutaendelea kuwahudumia hadi pale watakapokaa sawa huku tukiwaandalia utaratibu wa kuendelea na safari." Alisema Mh.Kemilembe.
Jitihada za kumpata kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ili athibitishe chanzo cha ajali hiyo bado zinaendelea na Matukio Daima APP inaendelea kufuatilia .
.…..... Mwisho...........
0 Comments