Header Ads Widget

WATUHUMIWA WA UKAHABA WAMDAI FIDIA BILIONI 36 DC WA UBUNGO

 


Sakata la watuhumiwa wanaodaiwa kufanya biashara ya kuuza miili yao (dada poa) waliokamatwa kufuatia oparesheni iliyoongozwa na Mkuu wa wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam Hassan Bomboko limeendelea kuchukua sura mpya baada ya hii leo, Alhamisi Juni 20.2024 jopo la Mawakili wa watuhumiwa hao wakiongozwa na Wakili Peter Michael Madeleka kutuma barua kwa Mkuu wa wilaya huyo kwa niaba ya wateja wao wakidai fidia ya Tsh. 36,000,000,000 (Shilingi bilioni 36 za Tanzania)


Kupitia barua hiyo yenye Kumb. namba SLC/HB/ 01/2024 Wakili Madeleka ameeleza kuwa madai ya fidia hiyo yanakuja kufuatia udhalilishaji waliofanyiwa wateja wao sambamba na kuwekwa 'rumande' pasipo sababu za msingi, ambapo amesema wateja wao (wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya dada poa) wameagiza kulipwa fidia hiyo ndani ya siku 14 kuanzia siku iliyowasilishwa barua hiyo


Imeelezwa kuwa kuanzia Juni 14 na 15 mwaka huu (2024) Mkuu wa wilaya huyo alitumia madaraka yake vibaya kwa kuwaita watuhumiwa hao 'dada poa', na kudai kuwa wamekuwa wakijihusisha na biashara ya 'ukahaba' kwenye eneo la 'Tip Top -Manzese' ambapo aliongoza oparesheni ya kuwakamata wadaiwa hao kutoka kwenye vyumba vyao na kuwapeleka kituo cha Polisi Mburahati ambako wamesota huko kwa takribani siku tano (5)

Barua hiyo imeendelea kufafanua kuwa ndani ya kipindi hicho Bomboko aliendelea kuagiza Jeshi la Polisi kutotoa dhamana kwa watuhumiwa hao jambo ambalo ni kinyume na Katiba na halikubaliki kwenye taswira ya sheria na ulinzi wa 'Haki za Binadamu', sambamba na hilo kufuatia maelekezo yake Juni 18 na 19 mwaka huu (2024) wateja wao walipelekwa kwenye Mahakama ya Hakimu mkazi Sokoine Drive, Dar es Salaam lakini hakuna mashtaka yoyote yaliyosomwa dhidi yao


Amesema malipo ya fidia ya Tsh. 36,000,000,000 (Shilingi bilioni 36 za Tanzania) inayodaiwa na wateja wao inatokana na hasara ya kiuchumi waliyosababishiwa, madhara yasiyo ya kiuchumi, maumivu na mateso, msongo wa mawazo, maumivu ya kihisia, kupoteza furaha ya kuishi, kushuka kwa sifa na hadhi nzuri kwa jamii waliyoitengeneza kwa muda mrefu, na kwamba malipo ya fidia hiyo yafanyike papo hapo.

CC:JamboTv


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI