Mahakama kuu kanda ya Iringa Imemuhukumu kifungo cha Maisha Jela Rashid Mwasema baada ya kumkuta na hatia ya kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin pipi 58 zilizokuwa na kilo 1.01 na dawa hizo zilikuwa tumboni.
Mwasema alikamatwa march 31 2023 alipokwenda kutibiwa katika kituo cha afya cha mtandika baada ya kuhisi maumivu ya tumbo na baadae alisema ukweli na kutolewa dawa hizo kwa njia ya haja kubwa.
Rashid Mwasema Mwenye umri wa miaka 37 alikuwa akisafirisha Dawa hizo akitokea Nchini Msumbuji kupititia Tunduma Na alipofika eneo la Ruaha Mbuyuni Wilaya ya kilolo alishuka na Kuelekea katika Kituo Cha Afya Cha Mtandika kutokana na Hali yake ya kiafya kuwa mbaya.
Baadae ya Taratibu za kumpima akalazimika kusema ukweli kuwa alikuwa amebeba dawa za kulevya tumboni ndipo taarifa zikatolewa Kwa Jeshi la Polisi na baadae Taratibu za kutoa pipi hizo zipatazo 58 Zikafanyika.
Kesi hiyo ilikuwa na mashahidi 11 akiwemo Daktari aliyesimamia kutolewa Kwa pipihizo,Mkemia Mkuu alethibizisha kuwa pipihizo ni dawa za kulevya Aina ya Heroin pamoja na Jeshi la Polisi waliohusika katika kumkamata.
Akisoma Hukumu Hiyo Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Iringa Ilvin Mgeta amesema Kuwa kutokana na ushahidobuliotolewa mahakamani hapo Ndugu Rashid Mwasema amekutwa na hatia ya Kusafirisha Dawa za kulevya na adhabu yake ni Kifungo Cha Maisha.
Kesi hiyo ilikuwa na waendesha mashtaka wa Serikali Magreth Mahundi na Yahya Misango waliomba Mahakama hiyo kutoa adhabu Kali Kwa mtuhumiwa Kwa Ili iwe fundisho Kwa wengine wenye Tabia kama Hizo Kwa Sababu dawa za kulevya zinaharibu Vijana na ndio nguvu kazi ya Taifa.
Kwa Upande wa wakili wa Utetezi aliomba mahaka kumpunguzia Mteja wake adhabu Kwa Sababu ni kosa lake la kwanza na Mteja wake Afya yake sio Nzuri.
Hata hivyo Mahakama ikamuhukumu adhabu Kifungo Cha Maisha Jela Ndugu Rashid Mwasemwa Kwa kosa la Kusafirisha Dawa za Kulevya Aina Heroin pipi 58 zilizokuwa na uzito wa kg 1.1
0 Comments