Header Ads Widget

WATOTO WENYE ULEMAVU WATAKIWA KULINDWA, KUUNGWA MKONO






NA HAMIDA RAMADHAN,MATUKIO DAIMA APP DODOMA

JAMII Imetakiwa kuwalinda na kuwaunga mkono watoto wenye ulemavu kwa kusimamimia haki zao na kuhakikisha maslahi yao yanalindwa. 

Hayo yanesemwa leo jijini hapa na Mratibu wa programu wa Taasisi ya Tanzania Foundation for Excellence in Disability ( TFED) Christina Mngara kwenye mkutano kuelekea siku ya mtoto wa Afrika. 


Amesema kwakufanya hivyo itawawezesha watoto hao kuwa watu wenye uwezo na ujuzi, pamoja na kujenga uzalendo kwa taifa la leo. 


 " Kwa kuzingatia umuhimu wa siku ya mtoto wa Afrika, tunapaswa kuendelea kuhamasisha ujumuishaji wa watoto wote katika elimu na jamii kwa ujumla, " Amesema . 


Na kuongeza "Kwa kutambua nafasi ya mtoto katika jamii yetu kama kaulimbiu ya mtoto wa Afrika mwaka huu ilitojikita katika kukuza elimu jumuishi, inayohusisha maarifa, maadili na Stadi za kazi tunaeelewa kwamba elimu Bora ni nguzo muhimu kwa ukuaji wa mtoto mwenye ulemavu na maandalizi ya maisha yake ya baadaye pamoja na kujenga taifa imara, " Amesema Mratibu huyo


Amesema  Taasisi hiyo ya TFED inalenga kuwawezesha watu wenye ulemavu pamoja na watoto wenye ulemavu kutambua na kutumia vipaji vyao ili kufikia malengo yao. 


Amesema siku ya mtoto wa Afrika ni siku Maalumu inayotambua na kusherehekea nafasi muhimu ya watoto katika jamii. 


" Hii ni siku ya kipekee inayotukumbusha wajibu wetu wa kuhakikisha kuwa kila mtoto bila kujali hali yake anapata fursa sawa za kuendeleza vipaji vyake na kufikia ndoto zake, pia niwashukuru wazazi na walezi kwani mmekuwa bega kwa bega katika malezi ya watoto hawa na kuhakikisha watoto hawa wanapata elimu Bora na msaada wanaohitaji, " Amesema


Kwa upande wake Afisa Elimu Msaidizi Mkoa wa Dodoma shule za Awali na msingi Tatu Mwangu amesema katika elimu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanawatambua watoto kupitia Serikali za Mitaa, walimu na kutoka sehemu wanazoishi. 


Pia amesema wamekuwa wakisadiana na wadau hao kuwaibua wale ambao jamii haijawaweka wazi ili kupata huduma. 


" Hivyo katika siku ya mtoto wa Afrika inakwenda kumpa faraja mtoto na kumpa nguvu mzazi au mlezi kwa kazi kubwa anayoifanya, " Amesema Afisa elimu huyo. 


Naye Mwalimu mkuu kutoka shule ya msingu ya Hombolo Beawani Paschal Ngoda Amesema katika jamii watoto wenye ulemavu ni kundi lililotengwa na kunyanyapaliwa hivyo yatupasa  kutambua suala la ulemavu sio la kumfanya mtoto kushindwa kufanya chochote. 


" Tuna kila sababu ya kuwapokea watoto hawa kwa hali yoyote na kutambua jamii hiyo ni sehemu ya jamii yetu na tuwape mahitaji yao ya msingi kulingana na hali za uhitaji wao, "amesema Mwalimu huyo. 


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI