WATANZANIA wametahadharishwa kuacha kuokota ovyo ndege wanaopigwa sumu na kufa kudai ni kwaajili ya matumizi ya chakula cha mbwa badala yake kwenda kuwala kwani kitendo hicho ni hatari sana kiafya.
Hayo yameelezwa na Meneja wa shirika la nzige la Africa mashariki la ukanda wa Afrika mashariki katika nchi ya Tanzania (Desert Locust Control Organization for Eastern Africa) Didas Joseph Moshi wakati wakiendelea na zoezi kuua ndege aina ya kweleakwelea kwenye mashamba ya wakulima wa Turiani wilayani Mvomero kwa kutumia ndege hiyo maalumu.
Akasema mara nyingi wakipita kukagua na kufanya tathmini ya ndege waliouawa kwa sumu hiyo Kwa kutumia ndege maalum, hukuta maeneo mengine kuna baadhi ya watu wanawaokota kwa wingi ndege hao na wengine wakitumia pikipiki kuwasafirisha.
Meneja huyo akizungumzia zoezi hilo la kuwadhibiti viumbe waharibifu wa mazao wakiwemo ndege hao, akasema Serikali imeokoa zaidi ya tani milioni 1.2 za mazao ya aina mbalimbali yaliyokuwa hatarini kushambuliwa na ndege hao katika kipindi cha miezi mitatu, Kati ya Machi hadi Mei mwaka huu.
"Kwa hesabu ya kifedha zilizookolewa ni takribani shilingi bilioni mbili za kitanzania au dola milioni moja za kimarekani, zoezi hilo lililohusisha mikoa ya Dodoma, Singida, Mbeya, Manyara, Morogoro, Shinyaga, Tabora, Kigoma, Mwanza na Mara bado linaendelea"Alisema Meneja huyo.
Akasema wamekuwa wakikabiliana na viumbe hai visumbufu vinavyohama kwenye nchi kwa kuhusisha mkoa kwa mkoa pamoja na kuhama baina ya nchi moja kwenda nchi nyingine.
Aidha akasema tangu kuundwa kwa shirika hilo miaka ya 62 Hadi sasa, Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi wanachama hivyo kufaidika na zoezi hilo na kwa hapa nchini viumbe waharibifu ambao wameendelea kupambana nao ni pamoja na nzige wa jangwani,ndege wanao haribu nafaka kama kweleakwelea,viwavi jeshi na mbun'go wanaoeneza magonjwa kwa mifugo
Meneja huyo wa DLCO-EA kwa Tanzania akasema katika msimu huu wa mwaka 2024 wamepata wimbi kubwa la ndege aina ya kweleakwelea hivyo shirika lilileta ndege tangu mwezi wa 3 na kuendelea na zoezi mpaka sasa
"Awali tulileta ndege moja lakini baada ya idadi ya ndege wavamizi aina ya kwelea kwelea kuwa kubwa tukalazimika kuleta ndege ya pili ili kuhudumia mikoa 10 ya Tanzania"Aliongeza
Akasema kazi ya kuua ndege sio kazi rahisi kutokana na ndege kulala maeneo tofauti tofauti wanayochagua hivyo huwawia vigumu kupiga dawa kutokana pia na kuwa na sheria pia zinazo kataza kupiga dawa moja kwa moja kwenye mazao ya chakula hivyo kulazimika kutafuta maeneo wanapolala ili kupiga sumu.
Akaongeza kuwa wamekuwa pia limekuwa likifanya kazi katika nchi zote 9 mwanachama na kwamba kwa mwaka huu tayari wamefanya kazi nyanda za juu kusini kwa mikoa ya mbeya,kanda ya kati yaani mkoa wa Singida na Dodoma, kanda ya Mangaribi kwenye maeneo ya kibondo, kanda ya ziwa katika mikoa ya Shinyaga Tabora na Mwanza na mkoa wa Mara ambapo kuna mazao ya mtama yanayo shambuliwa sana na Kwelea KWELEA.
Akasema Kwelea kwelea wamekuwa wakiongezeka kwa kuzaliana maradufu kutokana na uwepo wa mvua nyingi hasa zile za el nino zilizosababisha kilimo na mazao ya wakulima kuongezeka kwa kiwango kikubwa.
Alibainisha pia ndege hao aina ya kweleakwelea wamekuwa wakishambulia sana mazao ya umri wa saizi ya kati na chini likihusisha zaidi mazao jamii ya mpunga,ngano,uwele,mtama na ulezi ingawa mazao wanayoyapa kipaumbele kwenye uokozi zaidi ni mpunga kutokana na kulimwa katika kaeneo mengi.
Mmoja wa marubani wa ndege hizo Peter Lempatu akapongeza hatua ya Serikali kuweka ushirikiano na taasisi zake mbalimbali hali inayorahisisha utekelezaji wa zoezi la upigaji wa sumu.
Lempatu akasema kwa Tanzania wamekuwa hawakutani na changamoto kubwa sana kwakua mamlaka ya TPHPA wamekuwa wakirahisisha kazi yao kwa kufanya survey kabla ya marubani kufika,sambamba na kukuta huduma muhimu kama mafuta ya ndege na viuatilifu.
Nao baadhi ya wakulima, akiwemo Bi Salima Iddi,wakapongeza zoezi hilo kwa madai linaihakikishia nchi usalama wa chakula.
Mwisho
0 Comments