Header Ads Widget

THRDC YAONGEZA MKATABA NA PROTECTION INTERNATIONAL AFRICA KUKUZA UTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU

 


Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeongeza mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kushirikiana na shirika la Protection International Africa (PIA) katika harakati za utetezi wa haki za binadamu.


Mkataba huo una thamani ya Euro laki moja na ishirini na mbili elfu mia nne arobaini (€122,440).



Katika mkataba huo wa mwaka mmoja unalenga kuendeleza mradi wa kukuza nafasi ya kiraia nchini kwa kuimarisha ushiriki wa makundi yote ya Watetezi wa Haki za Binadamu (USAWA). 


Ambapo kupitia mkataba huo shughuli zinazokusudiwa kutekelezwa kwenye mradi huo zitachangia moja kwa moja katika kutekeleza malengo ya Mpango Mkakati mpya wa Mtandao ulioanza kutekelezwa 2023-2027.



Makubaliano hayo yamesainiwa rasmi Mei 31, 2024, na utekelezaji wake umeanza rasmi Juni 1, 2024, na unatarajiwa kumalizika Desemba 31, 2024. 


Mojawapo ya wanufaika wa mradi huu ni Watetezi wa Haki za Binadamu kutoka Tanzania bara na Zanzibar, wakiwemo watetezi wa haki za wanawake, watu wenye ulemavu, na jamii za kifugaji.


Mradi huo unatarajiwa kuongeza nguvu katika utetezi wa haki za binadamu nchini kwa kuboresha mazingira yenye usawa kwa jamii nzima.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI