.
Na Shemsa Mussa
Kagera.
Katika hatua za kuupokea Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka huu 2024 waratibu wa mbio hizo ndani ya Mkoa Kagera wameanza zoezi la ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri zote za Mkoa huo.
Akizungumza katika ukaguzi huo ulioanza kufanyika katika Wilaya ya Biharamlo,Bi Hellen Mbezi Mtaalamu na Mshauri wa Mbio za Mwenge wa Uhuru,amesema kuwa lengo la kukagua na kuitembelea miradi ni kutoa ushauri na kujua ni wapi pa kurekebisha na kutambua ubora wa utendaji kazi kwa wasimamizi wa miradi.
Amesema miradi iliyotembelewa ni miradi katika sekta ya afya , miundombinu ya Barabara ,Maji pamoja ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa katika Wilaya hiyo ,amesema licha ya kukagua miradi pia ukaguzi huo unazingatia umbari kutoka mradi mmoja hadi mwingine.
"Hapa Kagera nipo kwa kazi nyingi na hapa Biharamlo lazima tujikomboe ili tutoke kuwa nafasi ya mwisho na natamani Mkoa uje kuwa na nafasi ya kwanza katika kazi zote za Mwenge wa Uhuru,hivo lazima tupange ratiba nzuri na isiyochosha na miradi iwe Bora yenye viwango,amesema Bi Hellen"
Pia Bi,Hellen amewashauri Wakurugenzi,na wasimamizi wa miradi kufanya kazi kwa kushirikiana ila Kila kilicholegwa kiweze kukamilika kwa weledi bila kuleta mkanganyiko kwa wakaguzi na jamii kwa ujumla pia amewasisitiza kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa Mwenge wa Uhuru.
"Mwenge wa Uhuru ni jambo jema na la furaha siku zote tunatakiwa hapa Kagera tuutembeze Mwenge wa Uhuru na sio kuukimbiza,Mwenge ni furaha na faraja bwana ,na tuache visa na chuki katika kazi za Serikali na tukizembea tujue Maksi Moja ya wilaya ikidondoka basi jueni tunauangusha Mkoa mzima,ameongeza Bi,Hellen"
Mratibu Msaidizi wa Mwenge wa Uhuru Mkoa Kagera Bw Yasin Mwinory amesema Halmashauri zote za Mkoa zitatembelewa kwa ajili ya kuona miradi pamoja na kutoa ushauri wa nini kifanyike na kujipanga zaidi kwa ajili ya Mapokeo ya Mwenge wa Uhuru.
0 Comments