Header Ads Widget

WANANCHI MAKOME WAFURAHIA KUPATA HUDUMA YA MAJI


Na Mwandishi wetu, Matukio Daimaapp


Wananchi wa kijiji cha Makome wafurahia kupata huduma ya maji safi mradi ambao umezinduliwa na  kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Eliakim Mnzava .


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Mtwara Hamis Mashindike amesema kuwa mradi huo unaenda kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji katika vijiji viwili vya makome A na B.


Amesema kuwa mradi huo ulianza kujengwa Novemba 2023 na una tarajiwa kukamilika  Novemba 2024 ambapo unatekelezwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijjijini-RUWASA  Wilaya ya Mtwara.


Amesema kuwa mradi huo unajengwa kwa thamani ya  Shilingi milioni 600 fedha kutoka kutoka Wizara ya maji chini ya mpango wa lipa kwa matokeo (pforR) kwa utekelezaji wa kutumia mkandarasi m/s Kellogg constraction limited. 



Mradi huo umefikia asilimia 70 na unatarajia kuhudumia wananchi wapato 1,584  kati ya hao 858 wanatoka kijiji makome na 726 wanatoka katika kijiji cha makome B ambao ulianzishwa kwa lengo la kusogeza na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salam kwa wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara.

Mradi huu umehusisha ujenzi wa matanki mawili yenye ujazo wa lita 50,000 kwa kila moja  yenye mnara wenye mita 9 ambapo tenki moja limejengwa katika kiijiji cha makome B 


Mradi huu umehusisha ujenzi wa vioski 7 vya kuchotea maji, nyumba ya muhudumu, vyumba viwili vya kuwekea mitambo ya maji ya kupeleka umeme kwenye  chanzo cha maji ujenzi wa ofisi ya  chombo cha watoa huduma ya maji ngazi ya jamii(CBWSO), ulazaji wa bomba za maji umbali wa km4.1.


Aidha mradi huu umezingatia sera ya maji ya kumtua mama ndoo kichwani  na umezingatia umbali usiozidi mita 400 kutoka kituo kimoja cha kuchotea maji kwenda kingine.



Mradi huu utaongeza huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi kutoka asilimia 67.2 mwaka 68.2  mwaka 2023 hadi asiliam68,2 2024 mara ukapapo kamilika  ambap utatua changamoto  ya maji iliyokuwepo  awali katika kijiji hicho. 


Upatikanaji wa maji utasaidia kupungua kwa magonjwa  ya mlipuko katika jamii kutoana na matumizi ya maji safi na salam  hvyo kuchochea maendelea, na kutoa ajira za muda mfupi. 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI