NA MWANDISHI WETU
Lindi. Walimu ,wakandarasi na wafanyabiashara wamepatiwa elimi juu ya ulipaji kodi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Lindi pamoja na elimu juu ya kupambana na Rushwa.
Katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamalaka ya mapato mkoa Walindi wametumia semina hiyo kutoa elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi pamoja na kudai risiti wanapofanya manunuzi na kupinga vitendo vya Rushwa.
Meneja wa Mamlaka ya mapato (TRA) mkoa wa Lindi Matilda Kunenge amewaomba wadau hao kuomba risiti wanapofanya manunuzi katika maduka ili mapato ya serikali yasipotee.
"Unavyo ingia dukani ukinunua bidhaa udai risiti unapodai ndipo mapato yanaingia serikalini anapo kurudishia chenjia akupe na risiti inatakiwa itolewe hapo hapo ikitoka baadae ni makosa sio aende kuchukuwa kwenye duka la jirani.Pesa tunazokusanya ndizo zinazoenda kuijenga inchi."amesema Matilda Meneja wa TRA mkoa wa Lindi.
Meneja huyo wa TRA amewasisitiza washiriki wa semina hiyo kuwa kukusanya kodi ni jukumu la kila mtu sio wao peke yao.
"Watu wanafikiria kazi ya kukusanya kodi ni ya TRA pekeyao hapana ni yetu sote.Pesa tunazokusanya ndizo zinazo jenga inchi.Mtusaidie kwenda kutoa elimu, Tunaamini baada ya kikao hichi kila mtu ataenda kuanza kudai risiti."amesema Matilda meneja TRA
.
Matilda amewaomba wananchi wanapo uziana vyombo vya moto wafike kwenye ofisi za mamlaka ya mapato ili waweze kubadilisha umiliki.
Baadhi ya washiriki wa wameshukuru kwakupatuwa mafunzo waliyo yapata katika semina hiyo kwani imewaongezea uwelewa juu ya ulipaji wa kodi pamoja na mapambano zidi ya rushwa.
"Tumejifunza maana ya kupambana rushwa hasa kwenye miradi ya serikali Walamu hatukuwa uwelewa kwa sababu sisi sio wahasibu wala sio wataalamu wa manunuzi kwahiyo elimu tuliyo ipata leo itatusaidia sana.Tumepata uwelewa na miradi ya serikali itaenda vizuri.Kuna watu hawakuwa hata na uwelewa wa pesa zamiradi zinatoka wapi mishahara inatoka wapi kupitia semina hii wamepata uwelewa" amesema Frank Kapinga mwalimu shule ya Lindi Sekondari.
Naye Mvita Kangomba mfanya biashara amesema kwaelimu aliyo ipata leo amewashukuru TRA kwasababu hakuwa nayo awali.Amejifunza kuwa ni vyema wao wafanya biashara kuwa karibu na Mamlaka ya Mapato (TRA) amesema sikuwa na elimu hapo awali hasa hii ya mlipa kodi ameipata na ameelewa tukikwepa kodi anairudisha nyuma Inchi yetu na anaikwamisha serikali.
Kwaupande wake Kamanda wa Tasisiya kuzuiya na kupambana na rushwa (Takokuru) mkoa wa Lindi Asha Kwariko amesema tumewaita wadau ili tuweze kushirikiana nao katika jukumu la kuzuiya na kupambana na rushwa.
Kwariko amesema kupambana na rushwa ni jukumu la Watanzania wote sote tunatakiwa kushiriki kwenye haya mapambano.
"Kama Tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa Walindi tunafatilia miradi ya maendeleo inayo shugulikiwa na serikali tumebaini baadhi ya wakandarasi ama walimu hawalipi kidi ya zuiyo ama hawawasilishi TRA. Tumekubaliana tuite kikao kwanza tuwape elimu ya wajibu wao wakulipa kodi na wakuzuia na kupambana na rushwa pale wanapoona kuna vitendo kwenye manunuzi.Tumekubaliana na wenzetu wa TRA tuwape kwanza elimu elimu tukibaini kuwa bado wanatatizo la kutokulipa kodi au kuto wakata wakandarasi kodi ya zuiyo basi sisi tutaendelea na jukumu letu la kuchunguza pamoja na kufikisha kwenye vyombo vya sheria wale watakao kuwa wamejihusisha na vitendo vya rushwa."amesema Kamanda wa Takokuru mkoa wa Lindi Kwariko.
Mwisho.
0 Comments