Header Ads Widget

WAKULIMA WILAYA YA KYELA WALIA NA WEZI WA ZAO LA COCOA


TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII

Neema ya mfumuko wa bei kwenye zao la cocoa imegeuka karaha kwa baadhi ya wakulima Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya wamedai wanalazimika kuacha  makazi yao na kwenda kulala mashambani  wakilinda cocoa zisiibiwe na vibaka walioibuka baada ya  serikali kuliongezea  thamani zao hilo na kupanda bei.


Wakizungumza wakati wa ziara ya mbunge wa Jimbo la Kyela Ally Mlaghila ya kukutana na makundi mbalimbali ya wananchi kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero katika  kata ya Itunge ,wakulima hao wamesema baada ya cocoa kupanda bei ndipo wizi umeanza kushamili huku wanaofanya uhalifu huo wakifanya uhalibifu katika mashamba ya wakulima hao. 


Cocoa ni moja kati ya  zao  la biashara linalowaingizia kipato wakulima wa wilaya ya kyela mkoani Mbeya,

Wizi wa kokoa umeanza kulipotiwa maeneo mbalimbali mara Baada ya Bei ya Zao hilo kupanda kutoa shilingi elfu sita hadi kufikia shilingi elfu therathini kwa kilogramu moja.



Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kyela Ally Mlaghila amesema wako mbioni kuanzisha ulinzi shirikishi katika kata zote zinazokumbana na changamoto ya wizi wa kokoa huku akitumia nafasi hiyo kuwataka wanaofanya hivyo watafute kazi nyingine ya kufanya





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI