Mdau wa maendeleo Mkoa wa Iringa Aidan Mlawa (kulia)akikabidhi Vifaa vya michezo kwa timu zilizoshiriki mashindano ya Mlawa Cup
Na Matukio Daima App
Wadau wa michezo mkoa wa Iringa Wamepongeza jitihada kubwa za Kuibua Vipaji na kuuendeleza michezo zinazofanywa na mdau wa michezo Aidan Mlawa kwa timu za Mahenge wilaya ya Kilolo na kutaka wadau kama hao kuendelea kupongezwa
Enock Sikati katibu wa Mkwawa Queens asema hayo wakati akizungumza na Matukio Daima App kuwa mkoa wa Iringa tunahitaji wadau kama hao kwa ajili ya kuuendeleza michezo ili mkoa kuendelea kutangazwa kupitia michezo .
Alisema kwa kipindi ambacho mashindano ya Mlawa Cup 2024 yamefanyika taraha ya Mahenge kumekuwa na hamasa kubwa ya michezo na Wao kama wadau wa michezo wamevutiwa na jitihada zake.
Aidan Mlawa ambae amesomeshwa kwa debe la Pombe amekuwa mmoja wa Wana Iringa hususani wilaya ya Kilolo ambao wameendelea kurejesha fadhila kwa wananchi jambo ambalo ni jema na la kupongezwa zaidi.
Sitaki alisema wamevutiwa na jitihada zake na wanatamani kama angekuwa mkazi wa Iringa mjini .
Pia alimuomba Mlawa kusaidia timu ya Wanawake ya Mkwawa Queens ambayo inapambania kucheza lingi ya Taifa ya wanawake .
Katika mashindano yaliyomalizika hivi karibuni Aidan Mlawa alikabidhi shilingi Laki 5, jezi seti Moja na Mpira mmoja Kwa timu ya Magana Fc ambao walikuwa Mabingwa wa mashindano ya Mlawa cup huko Ruaha Mbuyuni.jana
Huku mshindi pili wa mashindano hayo Timu ya Mahenge Fc akipata shilingi Laki 2 jezi seti Moja na Mpira huku mshindi wa tatu akiwa ni Mbuyuni Fc ambayo walipata shilingi Laki 1 jezi seti Moja na Mpira.
Mara baada kukabidhi zawadi hizo, Mlawa aliahidi kutoa mifuko 60 ya saruji Kwa kila Kijiji kilichoshiriki mashindano hayo Mifuko 20 baaada ya kuombwa na mwenyekiti wa Kijiji Cha Mahenge Saidi Muhima kutoa Masada huo ili kusaidia ujenzi wa madarasa na Zahanati.
0 Comments