Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma
KAMATI ya mpito ya Kuratibu Uchaguzi wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserkali (NACONGO) imetoa wito kwa viongozi na wanachama wa mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs kujitokeza kugombea nafasi za uongozi wa baraza ngazi ya mkoa na uwakilishi wa makundi maalum na NGOs ya kimataifa.
Wito huo umetolewa jijini Dodoma na mwenyekiti wa kamati ya mpito ya kuratibu uchaguzi wa baraza la taifa la NGOs Christina Ruhinda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uchaguzi wa baraza la Taifa la mashirika yasiyo ya kiserikali kwa mwaka 2024.
Amesema kwa kufanya hiyo watakuwa wameleta maendeleo ya sekta ya mashirika yasiyo ya kiserikali nchini ambapo washindi wanatarajiwa kuapishwa Juni 11 mwaka huu.
Zoezi la kuchukua fomu za kugombea litaanza Juni 3 hadi 4 2024 huku fomu zitarudishwa Juni 5 hadi 6 2024, uchakataji wa fomu utafanyika Juni 7 hadi 8 2024 huku kampeni na zoezi la upigaji kura, kutangaza matokeo na kuapisha washindi litafanyika Juni 11, 2024.
Aidha Christina ameeleza Sifa za wagombea wa nafasi za uongozi pamoja na vigezo vya shirika kushiriki katika uchaguzi huo ikiwemo shirika liwe limesajiliwa kwa mujibu wa sheria ya ya NGOs sura ya 56 ya sheria za Tanzania.
Amesema mchakato wa uchaguzi wa baraza ngazi ya mkoa ambao utaenda pamoja na uchaguzi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, kimataifa na wawakilishi wa makundi maalum (Watoto, Vijana na Watu wenye Ulemavu).
Ametaja sifa za mgombea wa nafasi za uongozi kuwa anatakiwa awe kiongozi au mwanachama katika NGO iliyosajiliwa chini ya sheria ya NGOs na mwenye uzoefu na uelewa mpana wa sera, sheria, kanuni na miongozo ya NGOS, awe mtanzania isipokuwa kwa mwakilishi wa NGOs ya kimataifa lakini mwenye kibali cha kufanya kazi Tanzania, awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 70, asiwe alishawahi kupatikana na makosa ya jinai, awe na elimu ya kidato cha nne au zaidi, awe na uwezo mzuri wa kuzungumza lugha ya kiswahili na kiingereza na awe na akili timamu,”
“Vigezo vya shirika kushiriki katika uchaguzi liwe limesajiliwa kwa mujibu wa sheria ya NGOs, sura ya 56 ya sheria za Tanzania, liwe linatekeleza shughuli zake katika eneo au afua husika, liwe katika orodha ya msajili msaidizi wa halmashauri au Wilaya au mkoa husika, liwe linatekeleza shughuli zake kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo inayosimamia NGOs, ikiwemo ulipaji wa ada na wasilishaji wa taarifa na kila NGO lililokidhi vigezo tajwa hapo juu litakuwa na kura moja,"amesema Ruhinda.
Aidha ameeleza kuwa kamati wamejipanga kuhakikisha inapambana na kudhibiti viashiria vya rushwa kwenye uchaguzi wa baraza ngazi ya mkoa na uwakilishi wa makundi maalum.
“Zoezi la kampeni na kupiga kura wagombea watanadi sera zao kwa wapiga kura katika kila mutano wa uchaguzi, zoezi la upigaji wa kura litafanyika kwa siri, wapiga kura ni wawakilishi wa NGOs ziliyokidhi vigezo, wagombea wataonesha barua ya uthibitisho kutoka NGOs wanazoziwakilisha na nakala ya cheti cha usajili, wagombea katika ngazi ya mkoa ni wawakilishi watatu waliochaguliwa katika ngazi ya wilaya, uchaguzi wa makundi maalum utahusisha mwakilishi wa mashirika ya kimataifa na NGOs yanayotekeleza afua za watu wenye ulemavu, vijana na watoto,"alisema Ruhinda.
Ameeleza kuwa zoezi la kuchukua fomu za kugombea litaanza Juni 3 hadi 4,2024 huku fomu zitarudishwa Juni 5 hadi 6 2024, uchakataji wa fomu utafanyika Juni 7 hadi 8,2024 huku kampeni na zoezi la upigaji kura, kutangaza matokeo na kuapisha washindi litafanyika Juni 11, 2024.
Pamoja na hayo Kamati hiyo ya mpito ya kuratibu uchaguzi wa baraza la taifa la mashirika yasiyo ya kiserkali imetoa wito wa viongozi na wanachama wa NGOs kujitokeza kugombea nafasi ya ongozi wa baraza ngazi ya mkoa na uwakilishi wa makundi maalum na NGOs ya kimataifa kwa maendeleo ya sekta ya mashirika yasiyo ya kiserikali nchini.
Mwisho
0 Comments