UMMOJA wa Madhehebu ya Dini Mbalimbali kutoka Kata ya Mtera Halmashauri ya Wilaya ya Mpawapwa Mkoani Dodoma wamekutana na kuliombea Taifa huku wakiwataka watanzania kudumisha na kuitunza Amani ,utulivi na upendo uliopo.
Pia katika Kongamano hilo la maombi liliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mtera Dam walimuombea Rais Dkt, Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuliongoza taifa, kuombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu uwe wa Amani na haki.
Askofu Yona Njamasi katibu Mkuu Pentecost Bible Fellowship Church in Tanzania ( P. B. F. C. T) ambaye ni Mwenyekiti wa umoja wa madhehebu bonde la Mtera amesema Kongamano hilo ni mwanzo lakini wataendelea na magongamano mengine.
" Madhumuni Mkuu ya Kongamano hili ni Amani ndani ya taifa letu kwani pasipo Amani tusingeweza kuwepo hapa, tukumbuke Amani inaanza na MTU mmoja na kufuata mwengine na ikatoke Mtu mmoja akikosa amani kunahatari ya kufuata Mtu mwengine tuwe imara katika kuilinda na kuitunza Amani tulionayo, "
Awali wakisoma Risala yao mbele mgeni rasmi iliyowasilishwa na Mchungaji kutoka Kanisa la TAG Poniso Mgendela wameomba kupatiwa vipimo kwa ajili ya maabara,Vifaa vya X Ray kuongezewa wataalamu, kupatiwa gari la wagonjwa na pia kupatiwa vifaa vya mortuary ikiwa nipamoja jokofu.
Pia wameomba mradi wa maji ukamilike ili wananchi wapatiwe maji safi salama, kituo cha polisi kipatiwe majengo ya kituo nyumba za askari pamoja gari, ujenzi wa bwalo la shule ya Sekondari likamilike na pia hosteli ya wasichana ijengewe uzio kwa u salama wa wanafunzi pamoja na jiko la kidumu.
Kwa upande Mgeni rasmi katika Kongamano hilo ambaye ni Muelimishaji kutoka Ofisi ya Rais Ikulu Samweli Chimani amewataka wananchi wa Mtera kuwa na amani kwani changamoto zao zitafukishwa kama zilivyo kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassani na zitajibiwa hatua kwa hatua.
Aidha kuwa na imani na Rais Dkt Samia kwani ni Rais mwenye maona na upendo mkubwa kwa wananchi wake kwani ameweza kuendeleza na kuongeza zaidii yale yote yalioachwa na Rais wa awamu ya tano hayati Dkt,John Pombe Magufuli hasa mwenye miradi Mbalimbali ya kitaifa .
Hata hivyo amesema amefurahishwa na Kongamano hilo la kuliombea taifa liwe na Amani kwani Rais Dkt Samia Suluhu Hassani ni muumini wa amani na alipoingia madarakani aliomba amani kwa kuimarisha demokrasia na Uhuru kwa vyama vya siasa.
0 Comments