Na,Jusline Marco;Arusha
Kampuni ya Soil for future Tanzania ltd imesaini mikataba ya utekelezaji wa mradi wa kaboni ya udongo na kunufaisha vijiji vitano ambavyo ni Kimokouwa, Ngoswak, Sinonik, Loondolwo na Noondoto vilivyopo Wilayani Longido Mkoani Arusha ambavyo vimeweka jumla ya hekari 71656.30 kwa ajili ya nyanda za malisho ya mifugo.
Vijiji hivyo vitano kwa pamoja vimepata jumla ya shilingi milioni 372,326,135 kwa kuwezesha utekelezaji mradi wa ulishaji wa mzunguko wa haraka ambapo vijiji hivyo vilihitimu kujiunga na mradi wa Longido na Monduli Rangeland Carbon Project unaotekelezwa na kampuni ya Soil for the future Tanzania Ltd baada ya kusaini makubaliano ya hiari,mikataba,kupendekeza na kuwasilisha mapendekezo ya jinsi ya kutumia fedha zilizopatikana.
Mratibu wa mradi wa Longido Monduli Region and carbon project unaotekelezwa na kampuni ya soil for the future Richard Ndaskoi amesema kilichofanyika ni ulipaji wa malipo ya awali kwa vijiji vitano vilivyosaini mkataba wa kutekeleza mradi wa nyanda za malisho wa kaboni ya udongo unayotarajiwa kutekelezwa katika wilaya ya Longido na Monduli.
Ndaskoi amesema vijiji hivyo vitano vimepatiwa fedha hizo baada ya kukamilisha hatua zote na bafo wpo katika mazungumzo na vijiji vingine zaidi ya 20 ambavyo vimeshasaini makubaliano ya hiari ambapo katika utekelezaji wa mradi huo vijiji hivyo vitano vimeteua vijana watakaosimamia miradi hiyo na kushirikiana na kamati zao za nyanda za malisho katika kuhakikisha yote yaliyopangwa na kukubaliwa yanatekeleza kama ilivyotarajiwa.
Ameongeza kuwa mradi huo utatoa fedha kiasi cha dollar za kimarekani 2 kwa kila hekari moja ya ardhi iliyowekwa kwenye nyanda za malisho ikiwa ni malipo ya awali ya kuviwezesha vijiii hivyo kuandaa mipango na kuunda kamati za nyanda za malisho na kuzitumia pia katika kufanya mirafj ya kimaendeleo ambayo katika sheria za miradi ya kaboni Tanzania haipo ambapo baada ya hapo hewa ya kaboni itazalishwa na kuuzwa kulingana kwa kiasi kitakachozalishwa na malipo kuanza kipatikana kila mara wakati mauzo yatakapofanyika.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Marco Ng'umbi wakati akipokea hundi ya fedha hizo kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo kutoka kwa Kampuni hiyo na kuikabidhi kwa wenyeviti wa vijiji hivyo ameipongeza Kampuni hiyo kwa utekelezaji wa mradi wa hewa ya kaboni ya udongo katika wilaya hiyo ambayo imefuata taratibu zote kwa upande wa serikali,halmashauri na ushirikishwaji qa wananchi katika ngazi ya jamii.
Ng'umbi amesema fefha hizo zitasaidia katika upangaji wa nyanda za malisho kutokana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yanatishia utoweshaji wa sehemu za malisho kwa mifugo ambapo amewahakikisha wananchi wa Wilaya hiyo uwepo wa malisho bora na mifugo iliyo bora zaidi ambayo itainua uchimi wa mwananchi mmoja mmoja ambapo amesema ni lazima kupangilia na kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye kila kijiji unaoainisha maeneo ya malisho,maeneo ya makazi pamoja na maeneo mengine.
Ameongeza kwa kutoa rai kwa vijiji hivyo vilivyopokea fedha hizo kuzitumia katika malengo yaliyokusudiwa ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya pamoja na kuwajali wahitaji na kusisitiza matuzi bora na taratibu za fedha zifuatwe na fedha hiyo isitumike nje ya utaratibu wa taratizbu za kiserikali ambapo ameyataka makapuni mengine yanayohitaji kuwekeza Longido yatumie fursa hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido akizungumza katika makabidhiano ya hundi hiyo amesema hatua hiyo itatoa chachu kwa vijiji vingine kuiga mfano huo na itasaidia halmashauti na serikali kuu kujibu hoja za utekelezaji wa miradi ikiwemo afya kwenye maeneo ya vijiji hivyo,elimu kwa kujenga nyumba za walimu na kutatua changamoto hizo ambapo amewataka wenyeviti hao kufuata taratibu huku akiiomba pia ofisi ya mkurugenzi kufuatilia fedha hizo ili kuhakikisha zinaenda kufanya shughuli za kimaendeleo kwenye maeneo ya vijiji hivyo vitano.
"Na ninaamini kwamba vijiji wakisimamia fedha hizi vizuri ni matumaini yetu tutaenda kuzindua nyumba za watumishi wa afya na elimu kwasababu hizo ni changamoto kubwa sana kwenye maeneo yetu ya vijiji na tayati mikutano mikuu ya vijiji imefanyika na imeridhia juu ya uwepo wa mradi huu."Alisisitiza Ndg.Mollel Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo
Nao wenyeviti wa vijiji hivyo vitano ambavyo vimepatiwa fedha hizo wamelishukuru shirika hilo kwa utoaji wa fedha hizo ambazo zitaenda kuwasaidia katika kuboresha nyanda za malisho na katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya wananchi ambapo wameahidi kutoa ushirikiano kusudi kuweza kuisaidia jamii ya kifugaji.
Kelihery Emundoo kutoka Kijiji cha Ngoswak Wilayani Longido amesema kuwa kabla ya kupokea fedha za utekelezaji wa mradi huo walikaa kama viongozi wa kijijj hicho kuangalia namna ya kuisaidia jamii yao ambapo walikubaliana na shirika hilo kuamua kuwekeza kwao na kuisaidia jamii katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo shule,vituo vya afya na kusaidia walemavu.
Kwa upande mwingine Diwani wa Kata ya Noondoto Obedi Mollel ameishukuru Kampuni hiyo kwa kufanya moja kati ya vijiji vilivyomo kwenye kata hiyo kupata bahati ya kuingia ndani ya mradi wa Kaboni ambapo kimeweza kupokea zaidi ya Shilingi Millioni 84,viongozi wa kata hiyo walikaa kwa pamoja na kuanza kupanga matumizi ya kupeleka kwenye miradi ya kijamii ikiwemo uanzishaji wa wodi ya mama na mtoto katika hospitali iliyopo ndani ya Kata hiyo na ujenzi wa nyumba za walimu katika shule shikizi pamoja na ujenzi wa sekondari mpya ya Kata.
Katika suala la uboreshaji wa nyanda za malisho Ndg.Mollel amesema tayari wananchi wameshapata elimu na kamati za malisho zimeundwa na kuweka mpangilio mzuri wa malisho ya mifugo yao ambapo mpangilio huo ni utaratibu wa kawaida ambao unapaswa kufuatwa na kila mwananchi ili waweze kufaidika na kampuni hiyo.
Aidha miradi ya Kaboni ya udongo wa nyanda za malisho ni tofauti na mradi mingine ya kaboni kama vile kaboni ya misitu kwa sababu yenyewe huweka kaboni moja kwa moja kwenye udongo na hutekelezwa kwa ushirikiano wa kampuni ya Soil for the future na Halmashauri ya Wilaya ya Longido na Monduli.
Mradi huo unamanufaa ya moja kwa moja kwenye jamii kwani hutoa ajira kwa vijana ambao huajiriwa kama waratibu wa nyanda za malisho na kusaidiana na kamati za malisho za kijiji kusimamia ulishaji wa mifugo ambapo uboreshaji wa malisho ya mifugo na mapato kutokana na mauzo ya hewa ya kaboni unatarajiwa kileta manufaa mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.
0 Comments