Header Ads Widget

UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA VIJIJI NA VITONGOJI, NENDENI MKAGOMBEE TUTAWAUNGA MKONO



Na WILLIUM PAUL. 


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) amewasihi Vijana Wasomi wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Vijiji na Vitongoji 2024.


Ndugu Kawaida ameyasema hayo Wakati anazungumza na Wasomi wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam tarehe 16 Juni 2024 Karimjee Hall.



"Mwaka huu tuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Vijiji na Vitongoji lakini pia tuna Uchaguzi Mkuu 2025 na sisi Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tumekubaliana kuwaunga mkono kwenye Uchaguzi huu nendeni mkachukue fomu mtuachie kazi ya kuwasemea kwenye Vikao"

Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI