Header Ads Widget

TUMEPANIA KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI ZANZIBAR – DCP NG’ANZI

 


Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ramadhan Ng'anzi amesema Jeshi la Polisi linashirikiana na Taasisi nyengine zinazosimamia usalama barabarani kuweka mikakati ya kupunguza ajali za Barabarani ambazo zimekuwa zikileta madhara kwa jamii na Serikali. 



Akizungumza akiwa katika ziara ya kikazi visiwana Zanzibar amesema wamekubaliana na Mamlaka ya Usafiri na Usalama Barabarani Zanzibar kufanya Operesheni kwa madereva wa vyombo vya moto ili kuwadhibiti wanaokiuka sheria na taratibu za Usalama Barabarani.



Naye Mkuu wa Chuo cha Ufundi cha Arusha Technical Collage MUSSA CHACHA amesema  Chuo hicho kilatoa fursa za Masomo kwa watu wa Zanzibar hasa walimu wa vyuo vya udereva ili wawe na taaluma ya usalama barabarani na hatimae kupunguza ajali za barabarani.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri na Usalama barabarani Zanzibar HAJI ALI ZUBEIR amesema Mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na Chuo cha Ufundi Arusha ili kudhibiti ajali za barabarani hasa ajali zinazosababishwa na waendesha bodaboda.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI