Header Ads Widget

SUWASA YAWATUNUKU VYETI WANANCHI WALIOPISHA MRADI MAJITAKA SINGIDA




Na Thobias Mwanakatwe, SINGIDA 

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) imetoa vyeti kwa wananchi,kanisa na serikali ya kijiji Manga kwa kutambua na kuthamini mchango wao kutokana na kutoa maeneo yao kwa ajili ya kupisha ujenzi wa mradi wa mabwawa ya kutibu majitaka unaojengwa katika Manispaa ya Singida kwa gharama ya Sh.bilioni 1.7.


 Vyeti hivyo vilitolewa jana (Juni 5, 2024) na Diwani wa Kata ya Mtipa, Ramadhan Yusuph baada ya maafisa wa SUWASA kufika katika eneo la Manga kunapojengwa mradi huo kwa lengo la kutoa elimu kuwaeleza maendeleo ya mradi huo tangu ulipoanza kujengwa Mei 2023 hadi hivi sasa. 


Yusuph akizungumza baada ya kukabidhi vyeti aliwataka wakazi wa kata hiyo kuendelea kupokea na kufurahia miradi maendeleo inayotekelezwa ili kata ya Mtipa iweze kuendelea kwa haraka zaidi.



Naye Mhandisi Mazingira wa SUWASA, Richard Kasase  alisema ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 54 ya utekelezaji wake na shughuli mbalimbali za utekelezaji zinaendelea na unatarajia  kukamilika Novemba 2024. 


Kasase alieema kukamilika kwa mradi huu kutaboresha hali ya usafi wa mazingira katika Manispaa ya Singida na kuondoa umwagaji holela wa majitaka.


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SUWASA, Hosea Maghimbi aliwashukuru wananchi na Serikali ya kijiji cha Manga kwa kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa mradi huu tangu ulipoanza


Mwezi Machi mwaka huu, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, alipotembelea mradi huo aliiagiza SUWASA kuhakikisha wanasimaia mradi wa ujenzi wa mabwawa ya kutibu majitaka uili ujenga vizuri na uweze kulingana na thamani ya fedha.



Naye Meneja wa SUWASA,Sebastiani Warioba, alisema Mkuu wa Mkoa kuwa kujengwa kwa mradi huu ni ukombozi mkubwa kwa Manispaa ya Singida kwani kwa kipindi kirefu majitaka yalikuwa yakitupwa porini jambo ambalo kiafya sio zuri 


"Faida ya mradi huu kwa wananchi utawawezesha kupata huduma ya usafi wa mazingira kwa kuondoa majitaka kwenye makazi yao na kuongeza shuguli za maendeleo ikiwemo kuendesha kilimo cha mboga mboga," alisema.


Warioba alisema Singida imebahatika kuwekwa katika mpango wa mradi wa miji kumi ambao utawezesha kujengwa kwa mtandao wa majitaka kwa kujengwa kutoka kwenye majumba.


MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI