Header Ads Widget

UDAKTARI' WA RAIS DKT SAMIA SIO WA BAHATI MBAYA ILA ANASTAHILI

 


Na Gift Mongi MATUKIO DAIMA APP 

Moshi

Udaktari wa heshima ambao rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akipewa na takribani vyuo kadhaa sasa umeelezwa kuwa sio wa bahati mbaya na kuwa anastahili kutokana na mambo makubwa anayoyafanya.



Kwa kipindi cha miaka takribani mitatu tangu rais Dkt Samia Suluhu Hassan aingie madarakani kwa kuiongoza awamu ya sita tayari hadi sasa ameshapewa udaktari wa heshima na vyuo vitano tofauti vikiwemo vya ndani na nje ya nchi.


Miongoni mwa watanzania walioonyesha kukubali kazi nzuri zinazofanywa na rais Dkt Samia Suluhu Hassan nje na ndani ya nchi ni pamoja na mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro Prof Patrick Ndakidemi 


Katika taarifa yake kwenda kwa vyombo vya habari mbunge huyo amesema kuwa dunia imetambua juhudi za rais wetu katika kuimarisha uchumi wa nchi yetu na kuboresha mahusiano na mataifa rafiki.


Aliongeza kubwa  ametambulika kutokana na mabadiliko makubwa ya maendeleo aliyoyaleta kwenye sekta mbalimbali tangu alipoingia madarakani Machi 2021. 


'Kutambulika kwake kunatuongezea heshima  ya kimataifa na kuboresha diplomasia yetu ya uchumi wa kimataifa'ameeleza Prof Ndakidemi katika taarifa yake hiyo


Naye mkazi wa Kibosho Kirima Onesmo Mushi alisema rais Dkt Samia Suluhu Hassan anastahili tuzo hizi za udaktari wa heshima kwa namna ambavyo ameifungua Tanzania katika nyanja mbalimbali.


Alisema kwa sasa dunia inaijua Tanzania lakini hata sisi hapa nchini tumeshuhudia mambo mengi na makubwa yakifanyika hivyo heshima ya udaktari kwake sio bahati mbaya na anastahili.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI