Header Ads Widget

SUGU AANZA KAZI RASMI CHADEMA KANDA YA NYASA AKUTANA NA VIONGOZI WOTE IKIWEMO KAMBI MSIGWA

 TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII


Mwenyekiti mpya wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi Sugu Leo ameanza Rasmi kazi kwa Kuongoza kikao na viongozi wapya wa Chama hicho waliochaguliwa hivi karibuni .


Sugu amesema kuwa Leo ni Siku yake ya kwanza kufika ofisini .


"Siku ya kwanza ofisini... Leo nimeongoza kikao kazi cha Viongozi wakuu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Viongozi wote wa juu wamehudhuria akiwemo Makamu Mwenyekiti Frank Mwakajoka, Katibu wa Kanda Gwamaka Mbugi, Mtunza Hazina  Grace Shio pamoja na Wenyeviti wa Mabaraza yote akiwemo Mzee Charles Ndenga (Bazecha), Mama Tabia Mwaiteleke (Bawacha) na Vitus Nkuna (Bavicha)"amesema Sugu

Kanda ya Nyasa team kubwa ya viongozi waliopita ni kambi ya mchungaji Peter Msigwa aliyekuwa mwenyekiti wa kanda ya Nyasa ambae tayari amekata rufaa kupinga uhalali wa Sugu kuwa mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa.

Katika safu ya uongozi wa juu ya Chadema kanda ya Nyasa ni mwenyekiti wa Baraza la Vijana BAVICHA Kanda ya Nyasa Vitus Nkuna ndio anaingia kambi ya Sugu huko wengi Wao ni kambi ya Mchungaji Peter Msigwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI