Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe.Antony Mtaka akipanda mti aina ya Mvengi katika eneo oevu ndani ya kijiji cha Itengelo kata ya Saja Wanging'ombe
Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wakati Tanzania Ikiadhimisha siku ya Mazingira duniani Kila Juni 5 mwaka huu,Zaidi ya miti 3000 imepandwa katika maeneo mbalimbali Wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi huku Changamoto ya Uchomaji moto ikitajwa kuwa kikwazo kikubwa.
Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika Kimkoa katika Kijiji cha Itengelo kata ya Saja Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Antony Mtaka amesema wakati NEMC Ikipambana na kukabiliana na uharibifu wa mazingira lakini ni lazima hatua mbalimbali ziendelee kuchukuliwa dhidi ya moto kichaa.
Aidha Mtaka amesema katika kipindi cha miaka mitatu moto umeteketeza miti yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 100 katika maeneo mbalimbali na kulazimu kuelekeza kutungwa kwa sheria ndogondogo za vijiji za kudhibiti moto.
Awali Josia Murunya Meneja wa Baraza la mazingira kanda ya nyanda za juu kusini amesema kila mmoja anapaswa kulinda mazingira kwa kuhifadhi vyanzo vya maji na ndio maana wanaendelea kukapanda miti aina ya mivengi ambayo ni rafiki na vyanzo vya maji.
Wananchi wa Kijiji cha Itengelo mbali na kupongeza jitihada za utunzaji mazingira lakini wameiomba serikali kuwasaidia kutatua kero mbalimbali zinazowakabili zikiwemo za migogoro ya ardhi ambayo imekuwa mwiba mkali kwa muda mrefu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Mhe.Agnetha Mpangile anasema wilaya hiyo inaendelea kutatua migogoro hiyo ambayo imekuwa ikisababisha madhara kwa wananchi huku inayohusisha mkoa na Mkoa wakiuachia uongozi wa ngazi hiyo.
Matarajio ya wananchi ni kuona matatizo yao yanapatiwa ufumbuzi kwa haraka na mamlaka zinazohusika lakini kuchelewa kutatuliwa kuna sababisha chuki kwao.
0 Comments