Na Jusline Marco, Arusha
Wadau wa masuala ya watoto katika Hlamashauri ya Wilaya ya Meru Mkoani Arusha wameiomba Serikali kuanzisha malezi shirikishi kwenye jamii itakayosaidia kuigikia jamii kwa kutoa elimu ya malezi sahihi ili kuweza kujenga kizazi cha sasa na baadae katika maadili mazuri.
Wadau hao wametoa wito huo katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Juni 15 wilayani hapa ambapo imeelezwa kuwa karibu asilimia 70 ya tabia ya mtu hujengwa na malezi huku mmomonyoko wa maadili ukionekana kuwa chanzo cha uharibifu wa malezi na makuzi ya watoto katika jamii.
Mkurugenzi wa Aftican Hope Alive Tanzania Frank Elienea amesema kuwa mmomonyoko wa maadili unaweza ukaleta athali kubwa baadae endapo usipotafutiwa ufumbuzi sasa na kukakosekana vijana wenye kuacha alama sahihi.
Naye Iddy Ninga ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ya Dunia Salama amesema ukuaji wa teknolojia mtandaini hususani teknolojia ya habari na mawasiliano unapaswa utumiwe vizuri kwa manufaa ya baadae.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mashirika yasiyo ya kiserikali Halmashauri ya Meru na Mjumbe wa Baraza la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Mkoa wa Arusha Ndg.Vicent Ulega, kupitia siku ya mtoto wa Afrika amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanapata muda wa kutosha wa kukaa na watoto wao kuwaelekeza na kuwafundisha na kuweza kuwatawala katika masuala mazima ya kidigitali.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto katika halmashauri ya Wilaya ya Meru akisoma risala mbele ya mgeni rasmi amesema kuwa pamoja na elimu ya kipinga ukatili kwa watoto bado watoto wanakutana na changamoto ya kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kingono na watu wazima huku kesi za ibakaji na ilawiti kutupiliwa mbali kwa kukosa ushahidi wa kutosha ambapo mratibu wa masuala ya maendeleo ya jamii halmashauri ya Wilaya ya Meru amesema kauli mbiu ya mwaka huu inahimiza utoaji wa elimu inayojumisha watoto wote na inayolenga kumpatia mtoto maarifa,elimu bora,ufaulu,maadili mema na ujuzi pamoja na stadi za kazi ili kujenga ujuzi kulingana na umri wa mtoto.
Afisa Maendeleo ya Jamii,Dawati la Maendeleo ya Mtoto Mkoa wa Arusha Bi Hellen Materu akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bi.Emmanuela Kaganda 7amewataka wazazi na walezi kuwapatia watoto wao stadi mbalimbali za maisha ili kuweza kuwasaidia watoto wanaohitaji msaada ambapo ameahidi kushirikiana na viongozi wa halmashauri katika kutatua kero zilizowasilishwa na watoto.
0 Comments